Fredrick mwakalebela akizungumza kabla ya kutoa vifaa kwa kituo cha soka cha Iringa Football for hope kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki.(picha na denis mlowe iringa)
========  =========   =========
Na Denis Mlowe,Iringa.    
        
ALIYEKUWA Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, ametoa vifaa vya michezo kwa kwa shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Child Care (IDYDC) lililoanzisha kituo cha kukuza soka cha Iringa Football for hope kilichozinduliwa jana mjini hapa.

Mwakalebela alikabidhi vifaa hivyo kwa kwa mkurugenzi wa shirika hilo Johnnie Nkoma vikiwemo mipira kumi na mbili kwa ajili ya watoto wa kituo hicho, jezi seti moja, vuvuzela,filimbi, vikinga ugoko, beji ya nahodha, na Vitabu Kumi vya Soka la Tanzania alichotunga mwenyewe vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5.5

Mwakalebela alisema lengo la kutoa msaada huo kwa IDYDC ni kuunga mkono juhudi zao katika kukuza soka la watoto na vijana katika mkoa wa Iringa ambao unahitaji uhamasishaji wa kutosha kutoka kwa viongozi na wadau katika mkoa wa Iringa.

Alisema ataendelea kusaidia timu au asasi yoyote yenye nia ya kuendeleza michezo kwa mkoa wa Iringa na kuwataka wasisite kujitokeza wakihitaji msaada hata wa kimawazo.

  “Nawashukuru fifa na idydc kwa kuweza kuanzisha kituo hiki kwa watoto wa mkoa wa Iringa kwani kitawezesha kukuza soka katika mkoa na kuwataka wadau wengine kuwauunga mkono katika harakati za kukuza soka mkoa wa Iringa ambao uko nyuma sana kwa sasa” alisema Mwakalebela.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa IDYDC Johnnie Nkoma alimshukuru sana mwakalebela kwa kuonyesha mfano kwa kutoa vifaa hivyo na kuahidi watatumia katika kukuza soka la watoto kuanzia miaka 5 hadi 18.

Nkoma alisema lengo la kituo hicho kuwafikia watoto 8000 lakini kwa sasa wanauwezo wa kuchukua watoto 200 kutokana na kituo hicho. Aliongeza Iringa Football for Hope ni kituo cha kijamii chenye mlengo wa kulta mabadiliko na maendeleo kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Alisema kituo kinakusudia kutoa elimu ya afya kupitia mpira wa miguu na kuimarisha uwezo wa vijana kujilinda dhidi ya maambukizi ya virus vya ukimwi magonjwa ya zinaa na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Nkoma alisema kituo hicho kitakuwa kama jukwaa la vijana kuweza kukutana na kucheza michezo mbalimbali na kujenga mahusiano mazuri aidha kukuza vijapi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...