Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga wakati alipokua akitoa hotuba ya maelezo ya kitabu chake kipya cha cha Flames of Freedom Siku ya Jumanne Oct 14, 2013 ndani ya ukumbi Johns Hopkins Universi uliopo Jijini Washington D.C nchini Marekani.
Kitabu hicho kipya kilichapishwa baada ya uchaguzi mkuu uliopita, pia alizungumzia kua si mara yake ya kwanza kuandika kitabu cha wasifu wake kwani akiwa kizuizini alianza kuandika matukio aliyokuwa anayapitia lakini baada ya kuachiliwa akanyimwa makaratasi alivyokua kizuwizini.
Wasifu huo wenye kurasa 959 unaelezea maisha ya Bwana Raila Odinga kutoka utotoni hadi wakati alipohudumu kama waziri mkuu katika serikali ya muungano.
Raila Odinga wakati alipokua akiulizwa maswali na majibu na baadhi ya wanafunzi na wageni walikuwa wakati alipomaliza hotoba kuhusu Siasa za Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla, siku ya Jumanne Oct 14, 2013 ndani ya ukumbi Johns Hopkins Universi uliopo Jijini Washington D.C
Bw Raila Odinga ameelezea kuwa kitabu chake kina mchakato wa kupigania mfumo wa vyama vingi vya kisiasa nchini kwa ushirikiano na babake pamoja na rais mstaafu Mwai Kibaki. Ananukuu mateso aliyopitia wakati alipozuiliwa na rais mstaafu Daniel Moi kwa zaidi ya miaka mitano.
Wasifu huo pia unazumgumzia sababu zilizopelekea Bw Odinga kuungana na chama cha KANU baada ya uchaguzi wa 1997, njama za kumng’oa rais mstaafu Moi mamlakani kwa kutangaza 'Kibaki Tosha’ na jinsi alipoanzisha kampuni nyingi ikiwemo KEBS.
Raila Odinga alipokua akijibu maswali yalioulizwa na wageni walikwa pamoja na wanafunzi wakati alipomaliza hotoba kuhusu Siasa za Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla, siku ya Jumanne Oct 14, 2013 ndani ya ukumbi Johns Hopkins Universi uliopo Jijini Washington D.C
Odinga asema Uislamu ni dini ya amani, wakati alipokua akijibu swali kuhusu Al Shabaab Johns Hopkins Universi Washington DC.
BOFYA HAPA KWA PICHA NA VIDEO ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA NA VIDEO ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...