![]() |
Wema Sepetu akiwa na baba yake Balozi Isaac Sepetu siku alipotangazwa kuwa Miss Tanzania 2006. Kati ni mfadhili wa gari la zawadi alilopewa Wema kwa ushindi huo, Tanil Somaia |
Taarifa za awali zinasema kuwa,Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua.
Hadi Mauti yanamkuta,Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwa marehemu Sinza Mori jijini Dar es salaam, jirani na hostel za Chuo Kikuu.
Globu ya Jamii inaungana na Waombolezaji wote wa Msiba huu na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Mwenye Kurehemu, Aiweke Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu.
-Amen.
Papius: nakupa pole wema.
ReplyDeletePole sana Wema. Mungu akupe nguvu. Tumwombee mzee Sepetu apumzike kwa amani
ReplyDelete"INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN"
ReplyDeleteWEMA silie jikaze, POLE sana dada yetu,
MOLA umtangulize, ndo muweza kila kitu,
KIFO hata tujibanze, khatima ya kila mtu,
ILAHI PEMA MLAZE, ISAAC WA SEPETU.
Mwenyeez Mungu amrahamu, amughufirie kwa yote na amlaze pahala pema Peponi - AMEEN.
poleni sana wafiwa
ReplyDeletePoleni sana familia ya Balozi Isaac Sepetu pole sana Wema pamoja familia yote na dada na kaka zako wote. Pole my school Endita Sepetu. Rest in peace uncle Sepetu.
ReplyDelete