Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema ujangili wa pembe za ndovu na faru ni
tatizo la kimataifa linaolohitaji kutokomezwa kwa ushirikiano huku
akitaka mataifa makubwa kudhibiti soko la pembe hizo, hatua ambayo
amesema inaweza kukomesha uwindaji haramu unaoathiri utalii barani
Afrika.
Katika mahojiano amaaluma na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya
radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York, rais Kikwete ambaye pia
ameelezea hatari ya ugaidi nchini mwake na duniani kwa ujumla amesema
hata hivyo nchi yake imechukua tahadhari kujihami na mashambulizi
hayo.
Kwanza Rais Kikwete anaanza kufafanua ukubwa wa tataizo la uwindaji wa
pembe za ndovu na faru.
Raisi wangu nakushukuru sana kwa busara za kufikiria kutumia Jeshi letu ambalo ndo pekee linaonekana kuwa makini kati ya vyombo vya usalama.Binafsi ningeomba serikali ielekeze silaha zote kwenye Rushwa ambayo ndo mzizi wa kila kitu.Serikali inaonekana ina uwezo wa kufanya mambo mengi ilimradi kuna utashi,mf Kimbunga nk.
ReplyDelete