Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku wazee wa Njombe wakirusha njiwa kuashiria kuzinduliwa rasmi mkoa wa Njombe leo Oktoba 18, 2013 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Maisha Bora kwa Watanzania hajawezi kuja kwa watu kushinda wanacheza mchezo wa pool badala ya kujihangaisha kwa kufanya kazi na shughuli nyingine za kujiingizia mapato.
Aidha, Rais Kikwete ameahidi kuwa Serikali yake itakomesha haraka iwezekanavyo kero ya wananchi wa sehemu za Mkoa wa Njombe kulazimika kupanda mitini ili kupata mawasiliano ya simu za mkononi.
Rais Kikwete amayesema hayo leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Wanginyi, Kata ya Lupembe, Wilaya ya Njombe katika Mkoa Mpya wa Njombe kwenye siku yake ya kwanza katika ziara yake ya siku saba kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo.
Jamani Kikwete ni juu,, apewe heshima take
ReplyDeleteKikwete JUU ,JUU, JUU ZAIDI !
ReplyDeleteWenye wivu wajinyonge, muacheni Muungwana Jakaya mwana wa Tanzania.
Mkoa wenu wa Njombe umezinduliwa kwa heshima kubwa kabisa na Baraka na Mheshimiwa Raisi hadi kurushwa Njiwa weupe kitu ambacho Mikoa mingine haikupata!
ReplyDeleteIsiwe tena BARAKA ZA KURUSHWA NJIWA WEUPE ZIKAYEYUKA MKAANZA MIPANGO YENU YA AJABU KABISA YA KINYALU YA KUTAFUTA UTAJIRI KWA KUCHUNANA NGOZI NA MAUAJI YA MAALBINO!
Nkwel kabisa mnyonge mnyongeni haki yake mpeni... big up mr president JK
ReplyDeleteHivi tuna mikoa mingapi sasa Tanzania?
ReplyDeleteHongereni wana Njombe.
ReplyDeleteNaomba kujua tuna mikoa mingapi kwa sasa.