Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku wazee wa Njombe wakirusha njiwa kuashiria kuzinduliwa rasmi mkoa wa Njombe leo Oktoba 18, 2013 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe. PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Maisha Bora kwa Watanzania hajawezi kuja kwa watu kushinda wanacheza mchezo wa pool badala ya kujihangaisha kwa kufanya kazi na shughuli nyingine za kujiingizia mapato.

Aidha, Rais Kikwete ameahidi kuwa Serikali yake itakomesha haraka iwezekanavyo kero ya wananchi wa sehemu za Mkoa wa Njombe kulazimika kupanda mitini ili kupata mawasiliano ya simu za mkononi.

Rais Kikwete amayesema hayo leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Wanginyi, Kata ya Lupembe, Wilaya ya Njombe katika Mkoa Mpya wa Njombe kwenye siku yake ya kwanza katika ziara yake ya siku saba kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jamani Kikwete ni juu,, apewe heshima take

    ReplyDelete
  2. Kikwete JUU ,JUU, JUU ZAIDI !

    Wenye wivu wajinyonge, muacheni Muungwana Jakaya mwana wa Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Mkoa wenu wa Njombe umezinduliwa kwa heshima kubwa kabisa na Baraka na Mheshimiwa Raisi hadi kurushwa Njiwa weupe kitu ambacho Mikoa mingine haikupata!

    Isiwe tena BARAKA ZA KURUSHWA NJIWA WEUPE ZIKAYEYUKA MKAANZA MIPANGO YENU YA AJABU KABISA YA KINYALU YA KUTAFUTA UTAJIRI KWA KUCHUNANA NGOZI NA MAUAJI YA MAALBINO!

    ReplyDelete
  4. Nkwel kabisa mnyonge mnyongeni haki yake mpeni... big up mr president JK

    ReplyDelete
  5. Hivi tuna mikoa mingapi sasa Tanzania?

    ReplyDelete
  6. Hongereni wana Njombe.
    Naomba kujua tuna mikoa mingapi kwa sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...