Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Iringa jioni ya leo, Jumapili, Oktoba 13, 2013, kwa ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Iringa. Rais Kikwete amefuatana na Mama Salma Kikwete. 
 Shughuli kubwa ambazo Mheshimiwa Rais atazifanya wakati wa ziara hiyo ni kushiriki Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa mgeni rasmi katika Kilele cha Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu wa 2013 na Kilele cha Wiki ya Vijana. 
Ndege iliyombeba Rais Kikwete ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa kiasi cha saa 12.20 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wafuasi wa vyama vya siasa vikiwamo CCM na CHADEMA.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitakazofanyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Iringa mjini Mhe Msigwa katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitakazofanyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kamanda wa vijana wa CCM Mkoani Iringa,Mhe Asas katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitakazofanyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora. 
Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Are we really serious? Would be good to know what policies advocated by Mwalimu are still in place. Sisi watanzania ni wanafiki sana, tunamuenzi nini wakati sera zake zote tumeweka kapuni.

    ReplyDelete
  2. Nilisikia kuwa mjane wa Baba wa Taifa kaporwa kiwanja chake kule Msasani,Wabongo ndivyo tunavyomuenzi Baba yetu? Mungu aturehemu ili tuiogope dhambi! RIP Father of our nation!!!!!

    ReplyDelete
  3. Hivi huyu mwenyekiti wa vijana CCM anaitwa mhe. ASAS au anitwa Silim Jabir, ASAS si ni jina la viwanda vyao tu. Rekebisha hapo mkuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...