Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya jinsi Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa Bunge hilo. 

Bunge hilo Maalum la Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti ya Bunge la sasa lenye Wabunge 354 ambao ni pamoja na Wabunge 239 wa kuchaguliwa kutoka majimboni, Wabunge Wanawake Viti Maalumu 102, Wabunge wa kuteuliwa toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais.
Rais Kikwete akikaribishwa kutembelea Jengo la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo Oktoba 24, 2013.
Rais Kikwete akiangalia sehemu ya viti ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.
Rais Kikwete akitembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.
Rais Kikwete akisindikizwa na Naibu Spika Mhe Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.
Rais Kikwete akizungumza na Naibu Spika Mhe Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembeleaUkumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ili kupunguza gharama serikali haiwezi kutathmini matumizi ya teknolojia ya "teleconference" kwa kuunganisha kumbi mbili tofauti ili kupunguza gharama ya kung'oa viti na kuweka vingine na baadaye kungo'a tena?Au sheria kuhusu bunge inasemaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...