Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo na kulia pembeni ya Rais ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Joyce Kisamo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe walihudhuria uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwaeleza waandishi wa habari jinsi utafiti wa Gesi na mafuta unavyofanyika baharini muda mfupi baada ya kuzindua awamu ya nne ya Utafiti wa Gesi na mafuta uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Rais Kikwete aliwahi kuingoza wizara ya Nishati na Madini.Picha na Freddy Maro.
...''Raisi Kikwete aliwahi kuiongoza Wizara ya Nishati na Madini''...
ReplyDeleteKwa kweli Mhe. Raisi Kikwete zaidi ya kuwa Mwanadiplomasia na Mwana Uchumi, pia ni Mwanasayansi mzuri sana!!!
Tazama kwa uzoefu wake ktk Wizara ya Nishati na Madini anakuwa na uwezo Mkubwa wa kuwaelekeza Wana Habari kuhusu suala la Utafutaji wa Mafuta Baharini.
Acheni Mhe. Raisi Kikwete aitwe Dakitari !
ReplyDeletePicha a chini akishuka Kitaalamu na kwa kuzama kwa kina ktk suala la Mafuta Baharini.
Mhe. Raisi Kikwete hana Elimu ya kubabatisha kama wana vyodai Vilaza wachache!
ReplyDeleteHuyu mtu alizaliwa akiwa na akili zake timamu.
Je, ninyi mnaweza kuelewa Masuala ya Sayansi kwa undani kama anavyoshuka hapo chini ilhali mlisomea Uchumi na Diplomasia?
Safi sana.Vipi tumeshaandaa vijana lakini huko vyuoni?Ajira hizo.Hapo inahitajika School/college of Oil&Gas Exploration haraka sana.Nilisikia kinaanzishwa huko Mtwara(Street talks).Rais Kikwete majuzi wakati anahutubia kilele cha mbio za mwenge Iringa aliongea kitu muhimu sana...Sasa hivi tufanye mambo kwa kuangalia mbali zaidi,kwa kuwazia miaka 50,100 hadi 200 ijayo(akimaanisha vizazi vijavyo)
ReplyDeleteDavid V