Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua moja ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha vinywaji baridi cha Azam wakati Rais alipotembelea na kuzindua uzalishaji katika kiwanda hicho huko Mwandege, Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa waajiriwa wa kiwanda cha Bakhressa Food Products ambaye anaendesha fork lift Bi.Khadija Isihaka wakati Rais alipozindua uzalishaji katika kiwanda hicho kilichopo chini ya Kampuni ya Azam huko Mwandege,Wilyani Mkuranga leo.Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa zaidi ya watu 400.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi uzalishaji katika kiwanda cha Bakhressa Food Products huko Mwandege, Wilayani Mkuranga  leo asubuhi.Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Wapili kushoto ni mmiliki wa kiwanda hicho Bwana Said Salim Bakhressa na kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Abdallah Kigoda.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera JK kwa moyo mzuri ,ila viongozi waliopita walishataka kumfilisi mfanya biashara huyu bila makosa,leo hii asingekuwa hapo alipo.Ila Mungu amemsaidia kwenye lile balaa akanusurika.
    Kama inakumbukwa walichoma moto unga wa ngano kwa uzushi tu bila kuwepo na ukweli halisi wa makosa.
    Viongozi tuwape moyo wafanyabiashara wetu ,nchi yetu itajengwa na wananchi na sio wageni mnaowakumbatia kwa kupata ten/100.

    ReplyDelete
  2. Duh! Kumbe jamaa mwenyewe ndiyo huyu! Kwa kweli majivuno sifuri kabisa maana angekuwa mtu mwingine angekuwa anafahamika kwa kila mtu

    ReplyDelete
  3. Hongera Rais Kikwete, hongera Bakhresa.

    Hongera Rais Kikwete. Kufungua kwako kiwanda hichi kunaonyesha jinsi gani unathamini uwekezaji wa wananchi na unawapa moyo. Sio kila mara kuona miradi ya wawekezaji wa kigeni inazinduliwa.

    Hongera Bakhresa. Wewe ni pekee katika matajiri wanaowekeza sana katika nchi hii, wengine ni wavunaji na kupeleka nje.

    Kiwanda chako kimepunguza upotevu wa mazao, kinatoa ajira, kimepunguza matumizi ya fedha za kigeni kwa kununua juisi kutoka nje na kinaleta fedha za kigeni kwa TZ kuuza bidhaa zake nje.

    ReplyDelete
  4. Ona dada na hijab apiga kazi kama kawa.

    Dada wengine wadhani vazi hilo unatakiwa uwe mzembe tuu.

    Hongera Khadija.

    ReplyDelete
  5. Yaani kumbe ndo huyu MR BAKHRESSA
    dah pamoja na kuwa mzee wa bizness mkubwa lkn hata magazetini haonekani kweli hana majivuno wala mascandle Mungu akuongoze na moyo wako huo huo.

    ReplyDelete
  6. daa huyo jamaa haonekanagi ovyo.tangu nipo mdogo namsikia tu bila kujua yukoje.baadae bagamoyo kutakuwa hot,utakuwa mji uliotanuka kwa mambo mengi.viwanja kwa sasa bei poa tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...