Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua moja ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha vinywaji baridi cha Azam wakati Rais alipotembelea na kuzindua uzalishaji katika kiwanda hicho huko Mwandege, Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa waajiriwa wa kiwanda cha Bakhressa Food Products ambaye anaendesha fork lift Bi.Khadija Isihaka wakati Rais alipozindua uzalishaji katika kiwanda hicho kilichopo chini ya Kampuni ya Azam huko Mwandege,Wilyani Mkuranga leo.Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa zaidi ya watu 400.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi uzalishaji katika kiwanda cha Bakhressa Food Products huko Mwandege, Wilayani Mkuranga leo asubuhi.Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Wapili kushoto ni mmiliki wa kiwanda hicho Bwana Said Salim Bakhressa na kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Abdallah Kigoda.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.





Hongera JK kwa moyo mzuri ,ila viongozi waliopita walishataka kumfilisi mfanya biashara huyu bila makosa,leo hii asingekuwa hapo alipo.Ila Mungu amemsaidia kwenye lile balaa akanusurika.
ReplyDeleteKama inakumbukwa walichoma moto unga wa ngano kwa uzushi tu bila kuwepo na ukweli halisi wa makosa.
Viongozi tuwape moyo wafanyabiashara wetu ,nchi yetu itajengwa na wananchi na sio wageni mnaowakumbatia kwa kupata ten/100.
Duh! Kumbe jamaa mwenyewe ndiyo huyu! Kwa kweli majivuno sifuri kabisa maana angekuwa mtu mwingine angekuwa anafahamika kwa kila mtu
ReplyDeleteHongera Rais Kikwete, hongera Bakhresa.
ReplyDeleteHongera Rais Kikwete. Kufungua kwako kiwanda hichi kunaonyesha jinsi gani unathamini uwekezaji wa wananchi na unawapa moyo. Sio kila mara kuona miradi ya wawekezaji wa kigeni inazinduliwa.
Hongera Bakhresa. Wewe ni pekee katika matajiri wanaowekeza sana katika nchi hii, wengine ni wavunaji na kupeleka nje.
Kiwanda chako kimepunguza upotevu wa mazao, kinatoa ajira, kimepunguza matumizi ya fedha za kigeni kwa kununua juisi kutoka nje na kinaleta fedha za kigeni kwa TZ kuuza bidhaa zake nje.
Ona dada na hijab apiga kazi kama kawa.
ReplyDeleteDada wengine wadhani vazi hilo unatakiwa uwe mzembe tuu.
Hongera Khadija.
Yaani kumbe ndo huyu MR BAKHRESSA
ReplyDeletedah pamoja na kuwa mzee wa bizness mkubwa lkn hata magazetini haonekani kweli hana majivuno wala mascandle Mungu akuongoze na moyo wako huo huo.
daa huyo jamaa haonekanagi ovyo.tangu nipo mdogo namsikia tu bila kujua yukoje.baadae bagamoyo kutakuwa hot,utakuwa mji uliotanuka kwa mambo mengi.viwanja kwa sasa bei poa tu
ReplyDelete