Familia ya Kakore ya Dar es Salaam, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa watu mbalimbali waliofanikisha shughuli nzima za mazishi ya ndugu yetu mpendwa, Mwalimu Jasper Rashid Kakore (71), aliyefariki ghafla asubuhi ya Jumapili, Oktoba 20 na kuzikwa Jumatano Oktoba 23 mwaka 2013.

Shukrani ziwafikie wafanyakazi wote wa Kampuni ya Gapco Tanzania, Kika Contraction, New Habari 2006 Ltd, Wizara ya Fedha (Hazina) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Ukaguzi Kanda ya Mashariki), Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Pande, Wachungaji, Wainjilisti na watumishi wa K.K.K.T Usharika wa Mramba.

Pia wanachama wa Umoja wa Wanamtaa wa Tuna wa Dar es Salaam, Wanachama wa Umoja wa Wanakijiji wa Chome wa Dar es Salaam, Wafanyakazi wote wa Hospitali za Gonja, Apolo na Hospitali ya Wilaya ya Same, wafanyakazi na wanafunzi wa Shule za Sekondari Same na Dindimo.

Kadhalika tunapenda kuwashukuru Wanakijiji wa Gonja na Wanamtaa wa Vuje pia mitandao mbalimbali ya kijamii (Blogs) ndugu, jamaa na marafiki.

Tunaelewa kuwa watu ni wengi waliojitoa kwa ajili yetu hivyo kwa yeyote ambaye kwa namna moja ama nyingine hatukuweza kumtaja tunaomba radhi ila tunathamini sana kile ulichokitoa kwa ajili yetu.

Kama familia hatuna la kuwalipa ila Mungu aliyewapa moyo wa kujitoa ndiye atakayewarudishia mali na kila mlichotoa kwa ajili yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...