Mmoja kati ya Wakulima wa Kijiji cha Nguruweni Dole Mzee Kitwana Mustaha aliishukuru na Kuipongeza  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi kwa kukamilisha ahadi yake ya kuwapatia hati za umiliki wa mashamba  wakulima hao kwa ajili ya kilimo katika maeneo yaliyowahi kuleta mgogoro kwa muda mrefu.
  Baadhi ya wananchi na wakulima wa Kijiji cha Nguruweni wakiwa katika mkutano maalum  uliotishwa  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kukabidhiwa hati za umiliki wa mashamba ya kilimo katika maeneo yao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Nguruweni kabla ya kuwakabidhi hati za umiliki wa mashamba ya kilimo wakulima hao.
 Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Hati ya umiliki wa shamba Bibi Josephine Yohana kwenye hafla maalum ya kumaliza mgogoro wa mashamba katika kijiji hicho.
  Balozi Seif akimpatia Hati Bwana Mohd Ali Pili ya kumiliki eneo la kilimo katika Kijiji cha Nguruweni  ambako kuliibuka mgogoro uliosababishwa na kuinbgizwa watu wasiohusika na maeneo hayo kwa kilimo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...