Kwa mara nyingine tena Jumuia ya An Noor ya mjini Leicester nchini Uingereza
Iliwakaribisha Waislamu kutoka Leicester na vitongoji mbali mbali kusherehekea Eid el Adh-ha Jumatano ya tarehe 15 Oktoba 2013, Masjid An Noor iliyopo kati kati ya mji iliofurika waumini, wake kwa waume, na kuiachia Kamati Kuu ya
Jumuia ya An Noor changamoto ya kutafakari hali itakuwaje Inshaallah pale sherehe nyingine
za Eid zitapofanyika mwakani.
Msikiti ulijaa na kusababisha baadhi ya Waumini
kulazimika kuhamia misikiti ya jirani!
Pamoja na changamoto hizo, ni dhahiri kulikuwa na mazingira ya kupongezana si tu kwa sababu ya
Kusherehekea kukamilika kwa ibada ya Hijja, lakini pia kwa mafanikio ya jamii ya
Waislamu kutoka Afrika Mashariki kuweza kufikia malengo yake ya kuwa na kituo cha Kiislamu
Kati kati ya mji wa Leicester
Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi ya
Jumuia hii:
madrasatulnoor.01@gmail.com
au
Kwa simu:
Mwenyekiti- Mohammed Omar 44 7903 978481
Makamu- Abdul Dau 44 779 2104495
Katibu-Omar Hussein 44 756 5512058
kinachonikera hapo ni kufanya hotuba zenu kwa kiingereza wakati tunaojaa hapo ni watanzania.mbona misikiti mingine kama wahindi,wasomali na jamii zingine wanatumia lugha zao.tubadilike tukienzi Kiswahili chetu tuachane na mambo ya woga bila sababu.
ReplyDeleteUislamu ni chanzo cha umoja na mshikamano. Unapokereka mdau kwa kiingereza kutumika katika khutba za ijumaa katika msikiti ulioko Uingereza nashindwa kukushangaa.
ReplyDeleteJe kama mimi si mswahili unanambiaje?
Nisije kusali msikitini hapo?
Nilipohamia uk miaka ya tisini kulikuwa na tatizo hilo, lakini Alhamdulillaah ukiingia misikiti mingi ya waasia sasa lugha inayotumika ni kiingreza.
Uislamu ni mali ya kila muislamu, si dini ya majimbo.
Wala si ukabila.
Mdau Ukerewe
Namwomba Allah ujumbe huu umfikie mdau aliyekerwa na hotuba kufanywa kwa kiingereza wakati majority ni watanzania!
ReplyDeleteNi masikitiko kwamba bado waumini hayajajua hasa nafasi ya msikiti katika jamii ya kiislamu. Mdau anathibitisha hapo juu kuwa kwake yeeye msikiti ni kituo cha ukabila au utaifa.
Mdau dhana hiyo ni potofu sana na ni hatari kwa jamii ya Waislamu. Msikiti kamwe hauwezi kuchochea utengano baina ya watu. Msomali, mhindi, mwarabu wote mbele ya Allah ni kitu kimoja na inapotokea kuna aina yoyote ya ubaguzi inatakiwa Waislamu wapambane kwa hali zote kuuteketeza.
An Noor Community ya Leicester imeweka mikakati kuhakikisha kuwa kila aina ya muislamu anakaribishwa Masjid An Noor. Msikiti huu pia una Madrasah ambayo inatumia kiingereza kama lugha ya kufundishia. na hali ni hivyo hivyo inapokuja katika hotuba za Ijumaa, tunajitahidi kufikisha ujumbe kwa umma wa kiislamu. Kwetu kila muislamu ana thamani sawa, na sisi watu wa daawa tuna jukumu la kuwafikishia ujumbe kutoka kwa Allah. Na ndio maana msikiti unaoengeza idadi ya wazungumzaji wa lugha zingine si kuja kusali tu, bali hata kushirikiana nasi.
Mwenyezi Mungu atuongoze kuuelewa Uislamu kwa mujibu wa mafunzo sahihi, Amin
Mndengereko, Ukerewe