Katika Gazeti la Mawio Toleo Namba 0062 la tarehe 26.9.2013 – 02.10.2013 na toleo Namba 0063 la tarehe 03.10.2013 zimechapishwa habari zenye vichwa vya habari “Mtandao wa Ujangili Huu Hapa” na “Wabunge CCM watajwa ujangili”.

Katika habari zote hizo zimelihusisa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama chanzo cha habari hizo.

Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusiana na taarifa hizi:
  1. Shirika la Hifadhi za Taifa halijawahi kudhamini ripoti iliyotajwa katika habari hizo kuhusiana na utafiti makini wa ujangili.
  1.  Shirika husimamia shughuli za uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi    
           za Taifa pekee kiutendaji, ambapo baadhi ya maeneo yaliyotajwa  
           Katika habari hizo kama Selous na Liwale kiutendaji hayapo ndani
           ya Shirika la Hifadhi za Taifa.
  1. Kama Shirika la Umma, hufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kushirikisha vyombo mbalimbali vya dola katika kushughulikia uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo ujangili.

Ni kwa mantiki hii basi, shirika linapenda kuweka bayana kuwa halihusiki na taarifa hizo, na hata pale zinapopokelewa zina utaratibu wake wa kufanyia kazi. 

Tunachukua nafasi hii kuviomba vyombo vya habari kushiriki katika juhudi za kupambana na ujangili kwa kuwa waangalifu katika kuandika habari za kutuhumiana kabla ya kuwa na ushahidi kamili ambao ni haki ya kimsingi ya kisheria inayopaswa kuheshimiwa.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

07/10/2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...