KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI 

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.

MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JULIUS S/O MWAMBENJE, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA- UYOLE AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75.

MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. NYELAKOZI D/O MELANIA, MIAKA 33,,MKULIMA, NA 2. NDAISHIMILI D/O TEONYA,MIAKA 33,WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAKIWA NA WATOTO 11 AMBAO PIA NI RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LYIDIA D/O AMBAKISYE, MIAKA 25, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA LUPA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 5. 

MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAGUNGA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOHN S/O LUTIMBO, MIAKA 29, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4.

MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

DIWANI ATHUMANI - ACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu kamanda mbona anapenda herufi kubwa hivi? Jamani huko jeshini vipi? Mbona haya mambo yanafundishwa shule ya msingi. Katika vitabu vyote ulivyowahi kusoma primary, secondary nk nk, Je kamanda ulikwishapata kitabu ambacho kimeandikwa kwa herufi kubwa zote? herufi kubwa maana unapiga makelele.

    ReplyDelete
  2. Jamani! hii ripoti vipi.! Haya hebu mtuambie VIROBA SIYO GONGO? Tena hii inanywewa hovyo hovyo haijalishi uko wapi, hata ukiwa unaendesha chombo cha moto twende kazi kwa jinsi zilivyo nyingi na kila rangi sijui kama zinaubora. Msiwaonee hao wamama au kwa vile hazijawekwe kwenye vifungashio? Wengi wetu tumesoma kwa ajili mama zetu waliuza pombe Makamanda inabidi MKAZE BUTI, mtuondolee MADAWA YA KULEVYA ni aibu kwa Taifa letu!!! Watoto wa wenzenu mmewabandika majina MATEJA, wakamateni ili wawaonyeshe wanapoyanunu, sasa hivi muuzaji nani, yaani siamini kama mbinu zetu zote KWISHINEE.. Hali ni mbaya sana mitaani na kama hatua thabiti hazitachukuliwa basi kuna siku hata Rais wetu atapekuliwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...