Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Amin na Linah wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta kwa pamoja usiku huu,ndani ya viwanja vya Leaders club jijini Dar
 Baadhi ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Amin na Barnaba wakiimba kwa pamoja mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.
 Pichani juu na chini ni mwanamuziki Alain Laughton kutoka nchini Jamaica,akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la dar (hawapo pichani).  
 Mwanamuziki Alain Laughton kutoka nchini Jamaica,akiimba kwa hisia huku akipiga kinanda jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la dar (hawapo pichani).
 Mmoja  wasanii wa kike wa bongofleva aitwaye Recho, ambaye mara nyingi amekuwa akifananishwa na msanii aliyewahi kuwika kwenye anga ya muziki huo Ray C,pichani kati akilishambulia vilivyo jukwaa la fiesta na madansa wake.
 Mwanamuziki wa Bongofleva,Recho akiimba na mwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C usiku wa leo kwenye jukwaa la fiesta 2013,ambapo muonekano wake uliwashtua wengi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii H Baba akitumbuiza usiku huu mbele ya mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la serengeti fiesta linaloendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Leaders Club jijini  Dar,ambapo mashabiki kibao wa tamasha hilo wanaendelea kumiminika.
 Sehemu ya mashabiki wakishangweka usiku huu.
 Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Punguza mwili huo,kiuno cha nyigu kimepotea dada,hakionekani tena.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...