Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na ujumbe wa Tanzania wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na nchi mbalimbali duniani wakati wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Uhamiaji na Maendeleo . Mkutano huo ulifanyika mjini New York, Marekani tarehe 3 na 4 Oktoba, 2013 wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wengine katika picha ni Bibi Hannelore Manyanga (kulia), Kaimu Kamishna wa Uhamiaji kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Bi. Ramla Hamis, Afisa Mambo ya Nje.


Balozi Mushy akitoa hotuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kuhusu nafasi ya Tanzania katika kushughulikia masuala ya Uhamiaji na namna yanavyoweza kuchangia maendeleo ya nchi ambapo alitoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza majadiliano zaidi katika suala hili yatakayopelekea  kuunganisha dhana ya uhamiaji na maendeleo.
Kwa hotuba ya Balozi Mushy BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...