Pichani kulia ni Meneja wa Huduma kwa Jamii kutoka kampuni ya Tigo,Bi Woinde Shisael akizungumza mapema leo kwenye makao Makuu ya ofisi hizo kuhusiana na uzinduzi wa mpango maalum wa elimu ijulikanayo kama Elimu Mwanzo na Mwisho,yenye malengo ya kuinua kiwango cha elimu nchini kupitia sanaa na Mitindo ikishirikiana na Mfuko wa Elimu wa Bonnah Trust Fund.
Bi.Woinde alieleza kuwa,kampuni yake inatambua umuhimu wa elimu katika kujenga jamii yoyoye na ndio maana wameamua kushirikiana na mfuko wa elimu wa Bonnah Trust Fust kwa ajili ya kutoa mchango wao ili watoto waweze kuwa na uwezo wa kupata elimu bora nchini.Pichani kati ni Muasisi wa Mfuko wa Elimu ya Bonnah Trust Fund,Bi.Bonnah Kaluwa ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kipawa,jijini Dar es Salaam akiwa sambamba na Mratibu wa Matukio wa Onyesho la Wazi la mavazi na mitindo Bi.Regina Ogwal.
Muasisi wa Mfuko wa Elimu ya Bonnah Trust Fund,Bi.Bonnah Kaluwa ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kipawa,jijini Dar es Salaam akifafanua kuhusiana na kampeni hiyo,pia aliongeza kusema kuwa onyesho hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 12 jijini Dar,imeandaliwa mahususi kwa ajili ya kuinua elimu na kuhamasisha watu mbalimbali kuhusiana na sekta hiyo yenye changamoto mbalimbali nchini kupitia njia itakayokuwa na mvuto mkubwa zaidi kwa watu pamoja na kuburudisha kupitia onyesho hilo la mavazi,muziki na namna zingine za burudani zitakuwepo katika msafara huo utakaopita katika mitaa ya kusimama sehemu mbalimbali muhimu jijini Dar.Pichani kulia ni Msemaji Mkuu wa Bonnah Trust Fund,Bwan. Haji.
Saaafi sana tunaomba mfuko uwe endelevu ni wakati muafaka kwa wananchi kurudisha pesa kwenye jamii kwa ujumla watanzania wanaonyesha ufahari usio na maana kwenye arusi na kadharika badala ya shughuli za kimaendeleo kama hizi
ReplyDelete