Tume ya kikristo ya Huduma za jamii (CSSC), imezindua ripoti ya mradi wa Rasilimali watu (THRP), ambao ilikuwa inautekeleza kwa kipindi cha miaka 4 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha Huduma ya afya upande wa watumishi kwa kuwa na takwimu sahihi za watumishi wa sekta hiyo. CSSC imetekeleza mradi huo kwa msaada wa shirika la misaada la watu wa Marekani USAID kupitia shirika la IntraHealth.

Akizindua ripoti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Bw. Peter Maduki, amesema ripoti hiyo ina mambo mengi mazuri ya kujifunza ambayo yanatokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo. Katika ripoti hiyo jumla ya watu 146 wamefundishwa kuhusu mfumo wa kuhifadhi taarifa za watumishi wa afya kwa njia ya Kompyuta (HRIS), ambao ni watumishi wa CSSC, BAKWATA na APHFTA. Pia zaidi ya hospitali 70 zimefungwa mfumo huo kwa nchi nzima.

Uzinduzi huo wa ripoti, umekwenda sambamba na uzinduzi wa makala ya video (video documentary) inayoelezea mafanikio ya mradi huo.

CSSC imetekeleza Mradi wa THRP kwa kusimamia upande wa taasisi za dini na sekta binafsi, ikishirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA na umoja wa watoaji huduma za afya binafsi Tanzania (APHFTA). Kwa maelezo zaidi na kuona video tembelea; www.cssc.or.tz, www.afyamtandaonetwork.ning.com
Afisa Mradi wa THRP Bw. Renatus Sona akimkabidhi ripoti ya THRP Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Bw. Peter Maduki ili aweze kuizindua.
Sehemu ya watumishi wa CSSC na wawakilishi kutoka APHFTA na IntraHealth International wakishuhudia uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...