Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR), limeiomba radhi Serikali ya Tanzania kufuatia taarifa waliyoitoa
kwenye Mkutano wa 64 wa Kamati Tendaji (EXCOM) ya shirika hilo uliofanyika
Geneva, Uswisi tarehe 30 Septemba hadi tarehe 4 Oktoba, 2013. Katika taarifa
yao kuhusu Afrika, UNHCR ilieleza kuwa Tanzania imewafukuza Wakimbizi wa Rwanda
na Burundi katika operesheni ya kuwaondoa Wahamiaji haramu inayoendelea nchini.
UNHRC imeiomba radhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kupitia barua yake ya tarehe 2 Oktoba, 2013. Barua hiyo imeandikwa
na Mkurugenzi wa UNHCR Kanda ya Afrika Bw. George Okoth-Obbo (pichani) kwenda kwa Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano
huo unaofanyika kila mwaka.
Katika barua hiyo, UNHCR imeeleza kusikitishwa na
taarifa hiyo ambayo si ya kweli na imekiri kwamba Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana kwa karibu na UNHRC katika ngazi
zote kuhakikisha kwamba hakuna mkimbizi anayerejeshwa kwao katika zoezi la
kuwakamata na kuwarejesha kwao wahamiaji haramu linaloendelea nchini Tanzania.
Aidha, Bw. Okoth Obbo ameeleza kuwa UNHCR na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla inatambua
na kuthamini kwa dhati mchango mkubwa ambao Tanzania imeutoa na inaendelea
kuutoa katika kuwahifadhi wakimbizi wa mataifa mbalimbali kwa kipindi cha
takribani miaka 40.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea
kauli hiyo na kueleza kwamba inatarajia na inaamini kwamba UNHCR itaendelea kutoa
taarifa sahihi zenye kutoa picha halisi inayoonesha namna Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza wajibu wake kuwalinda na kuwahifadhi Wakimbizi kwa mujibu
wa Sheria za nchi na mikataba ya Kimataifa ambayo nchi imeridhia.
Mwisho.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
06, Oktoba, 2013
UNHCR wahakikishe huo waraka wa kuomba radhi wanausambazo duniani kote bila kuwasahau Rwanda, Uganda na Burundi ambao ndio waliwapotosha UNHCR. Hii itasaidia kusafisha jina la nchi yetu mbele ya mataifa mbalimbali na taasis zake.
ReplyDeleteNaungana na hapo juu. Kuiomba radhi Tanzania peke yake haitoshi. Kama ilivyokwamba taarifa hiyo potofu ilitolewa katika mkutano wa kimataifa, basi ni lazima dunia nzima itaarifiwe kuwa UNHCR walitoa taarifa ya uongo,na kujulishwa ukweli. UNHRC tayari wamechafua jina na nchi yetu. This MUST be a demand from Tanzanian government. Kuiomba radhi Tanzania doesn't remove the bad Picture that UNHCR has imposed on Our lovely Tanzania.
ReplyDeleteSielewi kabisa...wanaomba radhi kwani nani aliandika hiyo taharifa...what made them change their mind?
ReplyDeleteHaya mashirika hayana tofauti na NGO...uwepo wao unategemea uwepo wa wakimbizi...ndio maana wameamua kwa makusudi ku capitalize kwenye suala la sisi kuwafukuza wahamiaji haramu na ku twist dunia ione ni wakimbizi....
Na wanaomba msamaha serikali kama ujanja kwa maana kwamba walichoandika tayari kiko noted...watoe press conference tena CNN au media zote zilizotumika kutuchafua. Serikali isikubali hiyo huo msamaha...waiambie dunia kuwa wao ni wahongo...
Mdau (Mzalendo) The Hague
Kweli wajinga ndio waliwao. Kweli TZ imekubali hivi hivi wakati tayari dunia nzima imesikia hilo na kulaani,
ReplyDeleteNilishangaa Rwanda jeuri waliipata wapi ya kuanziasha chokochoko.
Huu waraka usambazwe dunia nzima. Tz sio wote mbumbumbu.
Msisahau kuna mtani wetu hapo anaitwa OKOTH.
ReplyDelete