Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa somo kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu namna wanavyoweza kutumia fursa zilizopo kupambana na umasikini na tatizo la ajira wakati wa mdahalo wa Wiki ya Vijana leo mkoani Iringa.
Mbunge wa jimbo la Mchinga Mh. Saidi Mtanda akizungumza na Vijana wakati wa mdahalo leo mkoani Iringa.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa leo kuhusu Wiki ya Vijana, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 zitakazofanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa . Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mi napata moyo sana nikiona serikali ya Dr kikwete wakihamasisha maendeleo kwani ndo njia pekee ya kulikomboa taifa. Kwa kweli kuna mwamko sasa hivi wa uhamasijaji na inafurahisha sana.

    ReplyDelete
  2. Tunahitaji watu wenye mbinu za biashara kuwahamasisha vijana waone fursa zilizopo badala ya kungoja za kupewa..Watanzania tuunahitaji kubadilika ilikuunga mkono wajasiriamali kwa kununua bidhaa zao ilikuchangia pato lao...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...