Ally Jakaya akifanyiwa interview
Mhandisi Magessa akielezea mfumo huo wa jua
======== ===== =======
Vijiji Bagamoyo kunufaika na umeme wa jua
Na Andrew Chale, Bagamoyo.
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi amewataka wananchi wa wilaya hiyo hasa vijijini kuchangamkia fursa ya kuweka umeme nuru utokanao na jua maalufu kama sola, ilikuboresha maisha yao na maendeleo kwa ujumla.
Kipozi alisema hayo mjini hapa juzi wakati wa hafla ya kufungua mafunzo maalumu ya umeme huo kwa mafundi umeme, wadau na wauzaji wa vifaa vya umeme na vijana mbalimbali ndani ya wilaya hiyo ambapo mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akielezea kufarijika na mafunzo hayo ndani ya Wilaya yake, Kipozi alisema “Ni fursa ya kipekee kwa wanamafunzo kutumia ujuzi huu kwani utaboresha maisha yenu na pia kwa vijiji vitanufaika na umeme huu wa nuru” alisema.
Na kuongeza kuwa, kwa fursa hiyo, anaamini matumizi ya kukata miti hovyo itapungua na baadala yake wananchi watanufaika na huduma hiyo endapo wataichangamkia. “Nawaomba wananchi hasa mulio vijijini kuchangamkia fursa hii ya umeme nuru, pia nawapongezeni wakufunzi na wandaaji kwa kuja muda muafaka kwani mafunzo haya ni mipango endelevu ambayo itasaidia kusambaza teknolojia ya nishati mbadala vijijini sambamba na kuwahamasisha wananchi kutumia nishati zitokanazo na teknolojia ya nishati jadilifu” alimalizia Kipozi.
Kwa upande wake, mkuu wa mafunzo hayo ya umeme nuru, Mhandisi, Finiasi Magessa alisema mafunzo hayo yatasaidia kuboresha maisha ya watanzania mbalimbali hasa wa vijijini ilikufikia malengo ya MKUKUTA, ili kila Mwananchi apate umeme wa uhakika na gharma nafuu ifikapo 2015.
Aidha, wanamafunzo wanatarajia kufaanya kwa vitendo kwa kufunga umeme nuru katika shule na nyumba za walimu za Sekondari Kiwangwa, Matipwili na Kibindu, huku mafunzo hayo yakitaraajia kumalizika Novemba Sab, mwaka huu.


Umeme wa jua sio wa mtu masikini. Matumizi ya nyumba moja tu basi si chini ya Tsh 15M ya vifaa vinahitajika. Kifaa cha kuwasha taa moja tu basi sio chini ya Tsh 100,000.
ReplyDelete