Na Hendrick Msangi
Ujumbe kutoka Norway unatarajiwa kutembelea nchini mapema mwezi Januari mwakani kwa lengo la kukutana na wananchi wa Mikoa ya Kusini na kujionea fursa za kiuchumi zinazopatikana katika Mikoa hiyo.
Ujio huo wa Wa-Norway umepangwa kufanyika kutokana na makubaliano baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mameya wa Miji ya Hammerfest na Sandnessjoen ya nchini Norway ya ushirikiano baina ya Miji hiyo na Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Katika Kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Oktoba 3 mwaka huu, iliafikiwa kuwa pande zote mbili yaani Wawakilishi kutoka Norway na wale wa Mikoa ya Lindi na Mtwara watembeleane ili kila upande upate fursa kujionea kwa macho fursa zilizopo kila upande ili hatua hiyo iwasaidie kufikia makubaliano katika vipaumbele vitakavyofaa kwa pande hizo kushirikiana.
Aidha, katika Kikao hicho kilichowakutanisha pamoja Mameya wa Miji ya Lindi na Mtwara, Wenyeviti wa Halmashauri za Miji hiyo, Balozi wa Norway hapa nchini Ingunn Klepsivik na Mwenyeji wao Profesa Muhongo, ilikubalika kuwa Wa-Norway ndiyo waanze kuja Tanzania na baadaye Wawakilishi kutoka Lindi na Mtwara nao waende Norway ili kujionea maendeleo yaliyofikiwa na Miji husika kutokana na kuzitumia vema fursa za kiuchumi zilizopatikana kufuatia uwepo wa rasimali za gesi na mafuta.
Balozi Klepsivik alisifu makubaliano ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili na kusema yatakuwa yenye manufaa makubwa na yatawasaidia wananchi wa Mikoa ya Kusini kukua kiuchumi na hivyo kujiletea maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
“Serikali ya Norway iko tayari kuwasaidia wananchi wa Lindi na Mtwara kwa kuwaelimisha na kuwashauri kuhusu namna bora ya kuitumia fursa ya upatikanaji wa gesi asilia katika Mikoa yao ili kukuza kipato chao na kujiletea maendeleo,” alisema Mheshimiwa Balozi.
Naye Waziri Muhongo aliwasisitiza Viongozi kutoka Mtwara kuanza maandalizi mara moja kwa ajili ya kuupokea ugeni huo hapo Januari mwakani.
“Haitapendeza waje hapa wakute hamjajiandaa, hakuna kitu cha kuwaonesha,” alisisitiza.
Kwa upande wao, viongozi kutoka Mikoa ya Kusini walioshiriki kikao hicho walimshukuru Waziri Muhongo kwa jitihada zake katika kuhakikisha wananchi wa Mikoa hiyo wananufaika na rasilimali ya gesi asilia iliyopo katika Mikoa yao.
“Tunakiri kuwa tumeitambua nia yako njema ya kutaka tunufaike na rasilimali hii,” alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi, Mathei Makwinya kwa niaba ya wenzake.
Mameya
wa Miji ya Mtwara na Lindi pamoja na Wenyeviti wa Halmashauri za Miji hiyo
wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye
suti-katikati), alipokuwa akifafanua jambo wakati walipokutana na Balozi wa
Norway nchini Tanzania, Ingunn Klepsvik, (kulia kwa waziri). Viongozi hao
walikutana Ofisini kwa Waziri, jijini Dar es Salaam, Oktoba 23, 2013 ikiwa ni
hatua ya awali ya kuanzisha ushirikiano baina ya Mikoa ya Kusini na Miji ya Hammerfest
na Sandnessjoen ya nchini Norway.
Balozi
wa Norway nchini Tanzania, Ingunn Klepsvik (wa kwanza kushoto) akimsikiliza kwa
makini Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Lindi, Mathei Makwinya
(aliyesimama), wakati Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
(hayupo pichani), alipowakutanisha Mameya wa Miji ya Lindi na Mtwara, Wenyeviti
wa Halmashauri za Miji hiyo pamoja na Balozi Klepsvik, Oktoba 3, 2013 ofisini
kwake jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ni kufuatia makubaliano yaliyofanyika
nchini Norway hivi karibuni kuanzisha ushirikiano baina ya Mikoa hiyo ya Kusini
yenye rasilimali za gesi na mafuta na Miji ya Hammerfest na Sandnessjoen ya
Norway ambayo imekua kiuchumi kutokana na rasimali hizohizo.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) na Balozi wa Norway
nchini, Ingunn Klepsvik (kushoto kwa waziri) katika picha ya pamoja na Mameya
wa Miji ya Mtwara na Lindi na Wenyeviti wa Halmshauri za Miji hiyo, mara baada
ya kikao chao kilichojadili hatua za mwanzo za ushirikiano baina ya Mikoa ya
Kusini na Miji ya Hammerfest na Sandnessjoen ya nchini Norway. Ushirikiano huo
umelenga kuzitumia fursa za kiuchumi zilizopo katika Mikoa husika hususan
rasilimali ya gesi asilia ili kuwaletea wananchi wake maendeleo na kukuza
uchumi wake. Kikao hicho kilifanyika Oktoba 3, 2013 Makao Makuu ya Wizara
jijini Dar es Salaam.
Norwegians have human face and integrity. I wish they are the ones to partner with Tanzania in exploring and exploiting our natural resources gas and petroleum in the south. We would benefit better
ReplyDeleteMkweli the Commentor above:
ReplyDeleteWe think that is what our 'good wishers' in the Tanzania Government are aiming about.
Better is to cope with them especially their state of art NORWEGIAN SOVEREING BOND or NORWEGIAN SOVEREIGN FUND or simply NORWEGIAN NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND for all citizens not only employed people.