Askari wa usalama barabarani wakijipanga kutoa huduma baada ya basi la daladala lililokuwa limebeba wanafunzi takriban 50 wa shule ya msingi ya Mgulani kugongana na gari dogo aina ya RAV 4 na kupinduka katika makutano ya Kenyatta Avenue na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam leo jioni. Dereva wa gari dogo akiwa na mtoto wa umri wa takriban miaka mitatu walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali. Wanafunzi wote walinusurika. Haijafahamika ni nini chanzo cha ajali hiyo ambayo basi lilikuwa likitokea kaskazini wakati gari dogo lilikuwa likitokea kusini.
 Uharibifu wa miundumbinu baada ya ajali hiyo
 Askari wa usalama barabarani wakiondoa mabegi ya wanafunzi hao ambao walitafutiwa basi lingine kuwapeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi
 Wanafunzi wakiwa katika gari walilotafutiwa baada ya ajali hiyo
 Magari ya break-down yakifanya juhudi ya kunyanyua basi hilo
Baadhi ya wanafunzi hao baada ya ajali. Ishukuriwe hakuna aliyeumia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mh jamani mbona hilo eneo ajali ilipotokea mtu huwezi kutegemea! Hizi ajali Bongo zinazidi sana. Mungu aiponye Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  2. Jamani, serekali inabidi ichukue hatua ya ziada kupunguza ajali Tanzania, ajali zimezidi sana hasa katika jiji la Dar es salaam, yani haid inaogopesha.

    ReplyDelete
  3. Uzembe, Haraka, Ulevi, Ubabe, gari bovu, dereva asiye elimika na asiye makini, nk. Haya tunajiletea wenyewe tusimhusishe Mungu. Tujirekebishe

    ReplyDelete
  4. Hawa vijana hawana dhambi bado. Mh!

    ReplyDelete
  5. Haya mambo tunajitakia wenyewe sisi watanzania, na tusipobadilika ndiyo yatazidi.

    Tatizo letu hatufikirii kabisa...watu tunadanganywa na makanisa kama EFATHA pale kwa Mwingira...akili tunaziweka makapuni...yaani watanzania sijui tumelaaniwa...

    Mwenye hilo gari kesho utasikia yuko EFATHA anafanya maombi badala ya kujiuliza kwa nini dereva wake kapata ajali na ni kitu gani kingeweza fanyika ajali isitokee..Vivyo hivyo kwa jamaa wa RAV 4 anatakiwa kujiuliza hayo maswali...Lakini hawa utakuta wapo pale kwa Mwingira..naye atawaambia hawajatoa fungu la kumi ndiyo maana wamepata ajali...basi ni biashara kwenda mbele.

    Mimi naona muda umefika kwa serikali kuyafungia haya makanisa maana yamekuwa chanzo kikubwa cha matatizo kwenye jamii...hayana tofauti na waganga wa kienyeji.

    Inabidi tutengeneze regulations za kuyadhibiti haya makanisa la sivyo juhudi nzuri za serikali na za raisi wetu mpendwa muheshimiwa Dr Kikwete zinashindwa kuzaa matunda kwa sababu ya watu kama Mwingira.

    ReplyDelete
  6. msemaji annonymous ya mwisho nikiwa naandika...(MB hatio time siku hizi??. Well said and need brave ppls to push katika hayo. nakubaliana naye 100% actually kama akipona na mtoto atapelekwa mbele ya TV na kueleza jinsi gani sadaka yake ilimuokoa??? believe me ..hata kama ni dini nyingine wanatumia hivyo. pls need taken serious. Ila ukweli ni kuwa hakuna uwoga wa kufuata sheria barabarani na watu hushinda kesi au kwa kuhonga au kujuana na watu...period! sasa hili haliji kwa kuomba watu wabadilike!!! linahitaji serikali inayoweza kuondoa haya! ..kazi kwetu wooote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...