Na John Nditi, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Oktoba 7, mwaka huu alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa kampeni ya upasuaji wa mtoto wa jicho , pamoja na kuwapatia huduma wagonjwa wanaishi na upofu utokanao na mtoto wa jicho.

Kampeni hiyo pia ililenga kutoa tiba kwa magonjwa mengine ya macho , na kuhamasisha wananchi kufuatilia huduma za macho bila kusubiri kampeni hizo , ambapo kampeni hiyo ilihusisha Wilaya ya Kilosa, Kilombero , Morogoro ( Manispaa) na Ulanga.

Hata hivyo katika kufanikisha kampeni huyo jumla ya madaktari watano kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Kilosa na Hospitali ya Mkoa wa Iringa waliweza kuwafanyia uchunguzi na jumla ya wananchi 12,080 walipatiwa matibabu mbalimbali.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Dk Godfrey Mtei, amesema mkoa imefanikiwa kupata wafadhili mbalimbali wanaochangia kwa kiasi kikubwa huduma hizo za macho .

Aliwataka baadhi ya wafadhili hao ni pamoja na International Islamic Relif Organization kutoka nchini Saudi Arabia , Humanitarian Relief Foundation kutoka nchini Uturiki, Bilal Muslim Mission, Lions Club ya Sweden, Sightsavers, Halmashauri za Wilaya na Serikali kuu.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kati kati ) akiwa na Mwakilishi wa Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Majed Al- Bagam ( kulia) pamoja na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Wariambora Nkya ( kushoto) , nyuma ( kushoto) ni Meneja wa Shirika la International Islamic Relif Organization kutoka Saudi Arabia, Majed Rashed , wakielekea kwenye hafla ya ufugaji wa kampeni ya upasuaji wa mtoto wa jicho iliyodumu wiki mbili kuanzia Septemba 25, mwaka huu mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akitoa hotuba ya kufunga kampeni ya upasuaji mtoto wa jicho.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania , Majed Al- Bagam , akisoma hotuba ya Balozi wake wakati wa hafla ya kuhitimisha kampeni ya upasuaji mtoto wa jicho.
Baadhi ya madaktari na watumishi wengine wakimsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( hayupo pichani).
Baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho wakati wa kampeni ya wiki mbili kuanzia Septemba 25, mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kaunda suti nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka nje na ndani ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...