Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakati wa uzinduzi wa baraza hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (kulia) akimkabidhi nyaraka za utendaji kazi mwenyekiti wa Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw. Omari Issa wakati wa uzinduzi wa baraza hilo leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw. Omari Issa akizungumza na wajumbe wa baraza hilo mara baada ya uzinduzi leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (katikati) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Baraza jipya la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw. Omari Issa (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Anacleti Kashuliza leo jijini Dar es salaam.
Wajumbe na Viongozi wa Baraza jipya la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...