
MAMBO
YANAENDELEA! Tamasha la wanamitindo na wabunifu walio katika vyuo vikuu
lijulikanalo kama ‘Redd’s Uni-Fashion Bash’, mwishoni mwa wiki hii
linatarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro, baada ya Mwanza kufungua
pazia.
Tamasha hilo linalochochea vipaji ndani ya vyuo hivyo,
mbali na Mwanza na Kilimanjaro pia litahusisha vyuo vilivyopo katika
Mikoa ya Dar es Salaa na Iringa.
Akizungumzia tamasha hilo,
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah alisema,
linatarajiwa kufanyika Jumapili ndani ya ukumbi wa Glessius uliopo mjini
hapa.
Fimbo alisema, wanafunzi wa vyuo vyote vya elimu ya juu
walio na mapenzi katika ubunifu na mitindo wanatarajiwa kushiriki
shindano hilo, huku akiamini kukiwa na upinzani mkali zaidi ya ule wa
Mwanza.
“Siku zote tunaamini katika kukuza vipaji zaidi, ila
siku hiyo kutakuwa na burudani kali kutoka kwa msanii Jon Makini,”
alisema Butallah.
Katika tamasha la awali lililofanyika Mwanza,
kulikuwa na ushindani mkali katika mitindo ambapo Fahad Rajab kutoka
Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) aliibuka mshindi akifuatiwa na Lucy
Charles kutoka pia chuo hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...