Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi Magdalena Mtengu (kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi kabla ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya wataalamu kuhusu kemikali zinazodumu katika Mazingira kwa muda mrefu,inayoanza leo mjini Arusha.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Dkt. Julius Ningu akifungua warsha ya mafunzo ya wataalamu kuhusu kemikali zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu,iliyoanza rasmi leo mjini Arusha, kushoto ni Muwezashaji katika warsha hiyo,Profesa Jamidu Katima wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya washiriki wa warsha hiyo.Picha na Evelyn Mkokoi, Arusha
Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto ya kuongezeka kwa maeneo yaliyoathirika na kemikali zinazokaa kwa muda mrefu zaidi ardhini.
Hayo yamesemwa leo Mjini Arusha na mkurugenzi wa idara ya mazingira kutoka ofisi ya makamu wa Rais Dkt Julias Ningu, wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya mafunzo ya wataalam katika utekeelezaji wa mkataba wa Stockhom ambao Tanzania ni wanachama.
Dkt. Ningu amesema kuwa, kutokana na ongezeko la matumizi ya kemikali zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Changamoto hii inazidi kuongezeka siku hadi siku kutokana na upungufu wa wataalam wenye ujuzi na vitendea kazi sahihi kwa ajili ya kusimamia kemikali hizi hususan mlundikano wa madawa ya kilimo yaliyokwisha muda wake.
Dkt. Ningu aliongeza kwa kusema kuwa, changamoto nyingine za kimazingira kwa sasa ni usimamizi wa kemikali hatarishi ikiwamo kemikali zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu ambapo suala hili linatokana pamoja na mambo mengine ukosefu wa ujuzi wa kutosha pamoja na miongozo sahihi ya namna ya usimamizi.
“Hii inaweza kusababisha hatari ya watu kuathirika kiafya hivyo, ni jambo la msingi kujenga uwezo wa wataalam wetu katika kusimamaia na kudhibiti kemikali hizi ili kulinda afya za watu na mazingira, Alisisistiza”.
Mkataba wa Stockholm ambapo Tanzania ni mwanachama, unazitaka nchi wanachama kuweka mfumo wa kitaasisi na kisheria katika kusimamia kemikali zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu, pamoja na kudhibiti madhara yake kiafya na katika mazingira.
Kwa kweli kwetu ni kama vile mazingira yanazidi kuchafuliwa! Na hili la kuchoma ovyo mifuko ya plastic? Huo moshi wake jamani ni mbaya sana au niseme unaweza kusababisha cancer! mifuko ya plastic inachomwa hovyo hovyo kwenye taka za majumbani, watu waelimishwe jamani na huo moshi wake una hizo gas ambazo ni POPs kwenye mazingira. Halafu haya mafriji yenye gas hizo yanaharibika na kutupwa hovyo hovyo, h´gas hizo sio nzuri na ni POPs. Mafuta ya transforma ambayo hutumika kupikia chips mitaani, nayo ni hivyo hivyo yana madhara makubwa. Mungu tu ndie anaweza kuwaponya watanzania na nchi yote, kwani kwa kutumia elimu zetu naona kama bado sana! nikilinganisha na nchi za wenzetu kwa kweli bado mno. Hongereni Mage kuhamasisha kwa kutoa mafunzo ya siku 2.
ReplyDelete