Washindi wanne kati ya  watano waliohitajika wa Chemsha Bongo ya kueleza tairi hili lilivyowekwa hapo wamepatikana baada ya wote kutaja kwa usahihi kwamba upande mmoja (usioonekana) wa hilo tairi ulikatwa kabla ya kuvishwa shinani. 

 Wadau wengi walijaribu (nasi tumewashukuru kwa kujaribu) na tunawapongeza sana, japo walikosea kusema kuwa tairi liliwekwa hapo tokea mti ukiwa mdogo. Ahsanteni wote kwa kushiriki.

Washindi wetu ni: Frank Msillu, 
Waheed Humoud, na amina Anita Daudi.

Tunaomba wadau mlioshinda mtupe anuani zenu kwa njia ile ile mliyojibia swali ili tufanye mipango kuwapatia  zawadi za T-shirt za Michuzi Blog 2014 mara tu zitapokuwa tayari.

Huu ni mwanzo tu wa michezo ya Globu ya Jamii ambayo imepania kutoa zawadi za hizo T-shirt kwa wadau mara kwa mara. Hivyo kaeni chonjo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kumbe na mie nilikuwa sahihi katika kutowa majibu yangu, ila sikuwa interested kuingia kwenye hicho kinyang'anyiro cha zawadi iliyoahidiwa. But still am so proud of myself lol.

    ReplyDelete
  2. Ni vizuri ukalidhibitisha hilo jibu lako kwa kuonesha huo upande uliokatwa kabla ya kuvishwa kwenye mti ili kuwalidhisha wote waliochukua muda wao kufikilia hiyo chemshabongo na sio kwa kutoa jibu rahisi namna hiyo.

    ReplyDelete
  3. The game is over!!

    ReplyDelete
  4. It is so obvious is it not? that is after the truth has been explained.This shows some of the amazing ways the human brain works. When confronted sometimes with a simple problem, we seek the complex explaination,we get flooded by our imagination.How often have we found out that our discoveries have always been around us, we just did not realise it.

    ReplyDelete
  5. Jibu hilo si sahihitairi hilo liliwekwa wakati mti huo ukiwa mche ili kuulinda lakini kwa bahati mbaya mti uliendelea kukuwa bila watu kufuatilia kulitoa tairi kwani haiingii mantiki ya kulikata ili kuliweka

    ReplyDelete
  6. Labda utuambie wewe mwenyewe ndo ulikata ukaliweka!!! maana inawezekana tairi liliwekwa tokea mti ulivyokuwa mdogo afu baada ya kukua likakatwa hapo pembeni kwa hiyo ukafikiri liliwekwa kwa kukatwa kumbe sio!!!!

    ReplyDelete
  7. Naomba tuoneshe kwa njia ya picha upande ule wa tairi uilokatwa.

    Pili, naomba utuambie washindi wanatoka nchi gani (wote wanaishi Tanzania)

    Mdau Ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...