Imeandaliwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha


Watanzania wakazi Uingereza wamehakikishiwa kuwa taaluma na uzoefu wao ughaibuni vitasaidiwa na vyombo husika vya serikali wakirejea na zana, mbinu na uwekezaji wa kilimo.

Kauli hii ilitolewa na msafara mzima wa viongozi uliofuatana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza alipokutana na Watanzania Ubalozini, London , Jumatano tarehe 23 Octoba 2013 .

“Malengo makubwa,” alieleza Waziri, “ ni usalama wa chakula na kujitosheleza kupanda mazao msingi kama mahindi, sukari na mchele. Tunachotaka ni maendeleo ya kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha biashara.  Nyinyi mnaweza kuwekeza katika uwezeshaji wa kilimo badala ya kununua kifaa kimoja kimoja.”

Akitoa mfano alisema Mtanzania aliyeshaishi ugenini anayetaka kuchangia atafanya bora zaidi kinyume cha kutafuta mbolea na kifaa kimoja, kimoja kuwa vifaa vikubwa ambavyo wakulima na jumuiya nzima vyaweza kukodisha.

Akifafanua zaidi Waziri Chiza aliyekuja Uingereza kwa mwaliko wa siku tano wa kiserikali alisema ni vyema Watanzania walioko ughaibuni kutafiti hali ikoje nyumbani. “Utafiti si kuingia mitandao ya Google na kujisomea tu. Njooni ubalozini maana hapa kuna habari za ukweli.  Serikali inaweza isijibu ombi la mtakaji haraka kama watu binafsi; hivyo ni vyema kufika ubalozini kupata habari za undani zaidi.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. HATURUDI NG'OOOO MLIMFANYA NINI TIDO MHANDO? MKIJA HUKU MNAJIDAI KUHMASISHA TURUDI WATU WAKISHAKUJA MNAANZA KUWALETEA ZENGWE NA SIASA ZENU KILA IDARA. BAKINI HUKO NA SISI TUKAE HUKU.

    ReplyDelete
  2. Kurudi nyumbani kusaidia kujenga nchi yetu takriban wengi wetu tunataka, ila nyie ndugu zetu ndio mnatuzuia na kutoruhusu uraia wa nchi mbili.

    ReplyDelete
  3. Laiti kama ujaji wa waziri huyu na dhamira ya mjadala anaouleta ungelitangazwa wengi tungelifika na kujadili issue hii.

    Ingawa waziri amegundua umuhimu wa sie tulio nje ya nchi juu ya taalamu na uzoefu wetu kwa nchi yetu. Hata hivyo sijui kama amewahi kusikia points zetu kuwa ili tuweze kuwezeka kiukweli hasa na kuweza kuwanufaisha watanzania na nchi yetu ni lazima uraia wa nchi mbili uruhusiwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimemaliza kusoma already na ninarudi back lets see kama kweli kazi zipo au ni ubabaishaji wakubebana kindungu

      Delete
  4. Mishahara ya watanzania wengine ni karibu milioni ishirini kwa mwezi mtawalipa hivyo wakirudi kutumikia taifa?

    ReplyDelete
  5. uraia wa nchi mbili wa nini???rudini nyumbani au mnaogopa maisha??maana mtu anaelilia uraia wa nchi mbili mara nyingi anaogopa maisha & amezoea kuishi kwa kutegemea benefits za bure za serikali wakati hajui kuwa ni kodi za watu wengine ndio zinamfanya aishi hivyo!

    Rais Mh JK na bunge la Tanzania naomba sana tafadhalini achaneni na hii non-sense ya kujadilia mambo ya uraia wa nchi mbili. Mtu alizaliwa nchi moja na anastahili uraia wa nchi moja full stop. Kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mtu na nchi ni bidii yake na si kutegemea ni raia wa nchi ngapi...Tz itasimama na kusonga mbele kwa raia wa nchi moja!

    Joe
    PhD student
    Canada

    ReplyDelete
  6. go to hell,turudi nyie mliokuwepo huko mnataka kutoka nendeni ngoja chimbeni mafuta kwanza tutakuja kama wajuzi wenye taaluma hiyo

    ReplyDelete
  7. Joe PhD. Student wa Canada naungana na wewe!

    Msitegemee urahisi kama mko tayari kuijenga Tanzania msinadi Uraia wa nchi mbili rudini Tanzania mfanye kazi!

    ReplyDelete
  8. Yaliyo mkuta Tido Mhando ni changamoto na sehemu ndogo tu ya maisha!

    Ni tukio la kawaida sana mabadiliko ktk sehemu ya kazi, kwani huko Majuu ninyi mpo kazini hapo hapo siku zote?,,,si mnabadili kazi na sehemu za kazi?

    Je, mbona Tido Mhando huku Tanzania yungali anaishi na hajakufa?

    Kwani huku Tanzania hivi sasa Tido Mhando hana kazi?

    ReplyDelete
  9. Yaliyo mkuta Tido Mhando ni changamoto na sehemu ndogo tu ya maisha!

    Ni tukio la kawaida sana mabadiliko ktk sehemu ya kazi, kwani huko Majuu ninyi mpo kazini hapo hapo siku zote?,,,si mnabadili kazi na sehemu za kazi?

    Je, mbona Tido Mhando huku Tanzania yungali anaishi na hajakufa?

    Kwani huku Tanzania hivi sasa Tido Mhando hana kazi?

    ReplyDelete
  10. Watu wanataka uraia wa nchi mbili ili wawe na uhuru ya kujiimarisha kiuchumi ndani na nje ya nchi. Si ndio wenzetu wanavyofanya ndio maana wanasonga mbele. Tanzania ina watu wengi sana wenye vipaji ila taifa isiporuhusu uraia wa nchi mbili hawa watu watazidi kukaa huko walipo.

    ReplyDelete
  11. Halafu kwa wanaotafuta kazi nawapa pole. Cha msingi na cha maana ni kujiajiri ukitoka nje ya nchi. Yaani anzisha kitu chako na uwaajiri wengine. Ukisubiri kuajiriwa utasubiri sana...labda uajiriwe na shirika au kampuni la nje halafu ubahartike kwamba wanakulipa vizuri kwa dola.

    ReplyDelete
  12. Kuna watu wanataka hela nyingi as if ukifanya kazi nje ya nchi unalipwa that much mnasahau kuna kodi na rent za kulipa nyumbani nyumbani tu hata kama unalipwa less

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...