Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwakaribisha nchini wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kabla ya kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda ambaye pia ni Mwenyekiti RECSA kwasasa, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (katikati). Dk Nchimbi anatarajiwa kuiongoza RECSA kwa kipindi cha miaka miwili. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Theoneste Mutsindashyaka. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (katikati) akizungumza na wajumbe wa RECSA (hawapo pichani) katika mkutano wao unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti RECSA ambapo anatarajiwa kuiongoza kwa kipindi cha miaka miwili. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Theoneste Mutsindashyaka. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (meza kuu-kushoto) anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake leo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (meza kuu-katikati).
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam kufunguliwa. Wapili kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (wakatikati). Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Silaha nyingi zinaazimwa kwenye vituo vya polisi.
    Bongo tambalale........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...