Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Wahamiaji (IOM) Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Ashraf El Nour alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa IOM nchini, Damien Thuriaux.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Wahamiaji (IOM) Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Ashraf El Nour alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa IOM alifika ofisini kwa Dk Nchimbi kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Wahamiaji (IOM) Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Ashraf El Nour kwa kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa IOM nchini, Damien Thuriaux. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Mhe. Dr.Nchimbi leooo Operesheni Kimbunga imetuponza Rwanda, Uganda na Burundi wametusemea IOM !!!
ReplyDeleteLa Muhimu ni kama ulivyo wafafanulia Ma-Bosi hao wa IOM ya kuwa Wageni Haramu hapa Tanzania walikuwa wanatumia hadhi ya Ukimbizi lakini wakiishi kwa Uhalifu na Ujambazi huku wakiwa hawafuati Kanuni na Sheria!
Mhe. Nchimbi ungewatolea hao Ma-Bosi uthibitisho wa ile Bunduki aina ya AK-47 aliyo kamatwa nayo ktk dari la nyumba yake Mkimbizi mwanamama kule Ngara.
Je, nchi gani duniani itakubali hivyo?
Ndio maana baada ya ufafanuzi Ma-Bosi wakatoa mikoni wakaaga na kuondoka!
Hao IOM hawajui ya kuwa ni muda mrefu saana nchi kama Rwanda, Uganda na Burundi zimekuwa na Serikali zao na Maraisi kamili na kuendesha Chaguzi Kuu nchini mwao mara kadhaa sasa hakuna Ukimbizi?
ReplyDeleteIOM !
ReplyDeleteMsaada usizidi uwezo, hao Wakimbizi wamekaa tokea mwaka 1959 wakizaliana na kujukuu nchini Tanzania na huku wakiwa na makundi kwa makundi ya mifugo na kutuharibia mazingira.
Enough is enough,
Let them go!
Tunaowarudisha kwao sio wakimbizi bali ni wahamiaji haramu. Naungana na mdau hapo juu, kama nchi zao zina serikali na hakuna vita wanang'ang'ania nini Tanzania? Na hao IOM ni wa ajabu sana kama hawataelewa umuhimu wa zoezi hili. Hata wao wana nchi ambazo zina sheria sifikiri kama watakubali tu sheria zao zivunjwe na wahamiaji haramu.
ReplyDelete