WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewaeleza washiriki wa Maonesho 14 ya Kimataifa ya China Magharibi kuwa Tanzania ni nchi ya pili duniani na ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na vituo vingi vya utalii na akawataka waanze kumininika kwa wingi kuja nchini kutalii.
Ametoa mwaliko huo leo asubuhi (Jumatano, Oktoba 23, 2013) wakati akihutubia kwenye maonesho hayo ya kimataifa yanayojulikana kama 14th Western China International Fairyaliyoanza leo jijini Chengdu kwenye jimbo la Sichuan, China na kuhudhuriwa na mataifa mbalimbali.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa mataifa 11 waliopata fursa ya kuhutubia maonesho hayo makubwa ya kimataifa, aliziomba kampuni za China kuja nchini kuwekeza kwa kujenga viwanda vingi vya nguo zinazotokana na zao la pamba.
Alitumia fursa hiyo pia kuinadi Tanzania kuwa ni nchi yenye ardhi kubwa tena yenye rutuba ambayo inafaa kwa kilimo, na kuzisihi kampuni za Kichina ambazo zinataka kuwekeza kwenye sekta ya kilimo zije nchini kwa ajili ya kulima kilimo cha mashamba makubwa ya biashara.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...