WAZIRI MKUU Mizengo Pinda anaondoka Dar es Salaam leo mchana (Jumanne, Oktoba 15, 2013) kwenda China kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo inayotarajiwa kuanza kesho, Oktoba 16.
Lengo la ziara ya Waziri Mkuu ni kutangaza fursa za uwekezaji hapa nchini, fursa za biashara, za utalii na kutafuta mitaji kwa ajili ya sekta zilizo chini mpango wa matokeo makubwa ya haraka (Big Results Now Initiative).
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Waziri Mkuu atakuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mhe. Li Keqiang na viongozi wa Serikali ya China katika katika sekta za uchukuzi, mawasiliano, viwanda, madini na nishati.
Atatembelea mji wa Beijing na majimbo ya Shenzen, Chengdu na Guangzhou ambako atakutana na Makamu wa Rais wa China, Rais wa Benki ya Exim ya China, Rais wa Benki ya Maendeleo ya China, wakuu wa mashirika makubwa na kampuni kubwa nchini China na kufanya nao mazungumzo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...