Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Likuyufusi iliyopo katika Kata ya Lilambo, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaambia wananchi wa eneo hilo kuwa, chama chake kimefanya makubwa kwa kujenga barabara, shule, pamoja na Zahanati tangu alipokuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akipimwa mapigo ya moyo na Afisa Tabibu, John Katundu baada ya kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Likuyufusi iliyopo katika Kata ya Lilambo, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Nachoa Zakaria. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaambia wananchi wa kata hiyo kuwa, chama chake kimefanya makubwa kwa kujenga barabara, shule, pamoja na Zahanati tangu alipokuwa mbunge wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia) akipokea zawadi ya kuku iliyotolewa na wapiga kura wake wa eneo la Likuyusi, Kata ya Lilambo, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaambia wananchi hao kuwa, chama chake kimefanya makubwa kwa kujenga barabara, shule, pamoja na Zahanati tangu alipokuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Wasanii wa Kundi la Star la mjini Songea mkoani Ruvuma wakitoa burudani ya kucheza na nyoka kabla ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia aliyevaa mawani) kuzungumza na wananchi wa kata hiyo kuhusiana na masuala mbalimbali ya maendeleo. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufunmiradi ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaambia wananchi hao kuwa, chama chake kimefanya makubwa kwa kujenga barabara, shule, pamoja na Zahanati tangu alipokuwa Mbunge wa jimbo hilo. Picha zote na Felix Mwagara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...