Waziri wa Nishati  na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipata maelezo kutoka kwa mhandisi wa usafirishaji wa njia kuu za umeme Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi Stanslaus Deogratias mara alipotembelea kituo kidogo cha kuzalisha  umeme cha Sumbawanga chenye uwezo wa kuzalisha megawati  5.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Sumbawanga mara alipotembelea kituo hicho.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wafanyakazi wa  Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Sumbawanga (hawapo pichani)  mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika wilaya hiyo. Waziri Muhongo amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi  kwa malengo ili kuchangia katika historia ya ukuaji uchumi kwa kutegemea nishati ya umeme.
 Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Sumbawanga wakifurahia  hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara baada ya kumaliza kikao na wafanyakazi hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mheshimiwa kazi yako ni tukufu.Tatujaona mgao 2year ukiwepo ni matatizo ya kiufundi kweli tulikua tukihujumiwa hongera sana na mungu akulinde uishi siku nyingi.enzi hizo kipindi kama hiki mvua hazijanyesha ingekua kasheshe hakuna kusikilizana.

    Viongozi tubadirike tuache ubinafsi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...