Na Tamimu Adam - Jeshi la Polisi.
JESHI Polisi Mkoani Mtwara  limefanikiwa kukamata  gari lenye namba za usajili T.867 aina ya Toyota Carina Saloon likiwa limebeba  shehena ya mifuko  yenye meno ya Tembo tisini (90)  yenye uzito wa kilogramu 222.1 ya thamani  zaidi ya  shilingi bilioni moja (1,082, 025,000/=)
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Steven alisema kuwa gari hilo lilikamatwa kata ya Maendeleo, wilaya ya Masasi katika barabara kuu ya Tunduru kuelekea Masasi.
Zelothe alisema kuwa askari wa doria walilitilia shaka gari hilo na kumuamuru dereva  kusimama kuonyesha leseni  ya udereva ambapo dereva wa gari hilo hakuwa nayo, ndipo askari alichukua hatua ya kufanya ukaguzi ambapo alikuta gari hilo limejaza shehena ya mifuko inayosadikiwa kuwa ni meno ya Tembo.
 “Askari waliamua kulifisha gari hilo kwenye kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Masasi umbali wa kilometa moja kutoka sehemu lilipokamatwa gari hilo, wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni dereva na mwenzake walikuwa wakimshawishi askari huyo waelewane ili wampatie shilingi milioni tatu aweze kuwaachia lakini askari huyo alikataa na kufanikiwa kulifikisha gari hiyo kituoni” Alisema Zelothe.
Alisema kuwa kabla gari hilo halijasimama vizuri dereva na mwenzake waliruka na  kutokomea vichochoroni, juhudi za kuwasaka bado zinaendelea ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Miongoni mwa vitu vilivyokutwa ndani ya gari hilo wakati wa upekuzi ni pamoja na simu moja ya kiganjani aina ya Techno, mizani aina ya tonash, fomu za “notification” pamoja na Bank slip.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Aya ..yaya

    ReplyDelete
  2. Haya tunaomba hao wahusika wa nyongwe mpaka kufa coz hawalitakii mema taifa letu,,na huyo polisi wapandishwe cheo haraka sn coz tunataka uzalendo kama huu,,naitwa mdudu kakakuona,,nipo huku UINGEREZA,,amani kwa taifa langu amani kwa watanzania wooote,,but not to MIJANGIRI-li really I hate them stupid people,

    ReplyDelete
  3. MBONA OPARESHENI UHAI ILIYOHUSISHA JWTZ NA KUFADHILIWA NA UINGEREZA MIAKA YA TISINI ILIFANIKIWA KUKOMESHA UJANGILI SASA KIGUGUMIZI HIKI CHA SASA KINAONESHA DHAHIRI UHUSIKA WA VIONGOZI KWENYE UJANGILI. RAIS, WAZIRI NA WANANCHI WOTE SISI TUNALALAMIKA SIJUI KWA NANI! AFRIKA KUNA VITUKO.

    ReplyDelete
  4. jamani haiingii akilini watuhumiwa kutoroka mikononi mwa police!!eti gari halijasimama vizuri wakaruka maana yake ninini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...