Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali akiwashukuru wageni waalikwa wakiwiwemo Waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi mbalimbali kutoka bara la Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwa kufika kwao kwenye chakula cha jioni Fairmont Hotel iliyopo Washington, DC walichomuandalia mwanamuziki maarufu kutoka Afrika ya Kusini, Yvonne Chaka Chaka kwa heshima ya kuwa Balozi wa kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa malaria Barani Afrika. Balozi Amina Salum Ali aliwashukuru Benki ya Dunia kwa juhudi za makusudi wanazofanya kuhakikisha Bara la Afrika linatokomeza kabisa gonjwa hili hatari la Malaria, pia Balozi Amina Salum Ali alimshukuru Bwn. Tim Ziemer kutoka USAID kwa jitihada zao za kupigana kuutokomeza ugonjwa wa malaria Duniani hususani Bara la Afrika.
Kushoto ni Mwanamuziki wa Afrika ya Kusini Yvonne Chaka Chaka akifuatilia hotuba ya Balozi wa African Union Mhe. Amina Salum Ali, kulia ni Kaimu Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Marekani Mhe. Johnny Moloto.
Kutoka kushoto ni Mhe. Balozi wa Swaziland Rev. Dr. A. M. Ntshangase, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Balozi wa Botswana nchi Marekani Mhe. Dr.Tebelelo Mazile Seretse.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Nafikiri kuna makosa na huwa yanafanyika mara kwa mara. Hakuna Balozi wa kudumu ila kuna Ubalozi wa kudumu wa Umoja wa nchi za Africa (AU), so as ubalozi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa. Ubalozi ndiyo wa kudumu siyo balozi. Kwahiyo ingesomeka hivi: Balozi wa Ubalozi wa kudumu wa Umoja wa nchi za Africa (AU) Mheshimiwa ....Haya makosa nimeyaona mara kadhaa...just so next time msiwape hawa watu ubalozi wa kudumu.
ReplyDelete