Mahmoud Ahmad Arusha

Mkutano wa siku mbili wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa kwamba Ziwa Manyara lipo hatari ya kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uharibifu wa mazingira kunakotokana na kilimo pembezoni mwa mito kama juhudi za maksudi hazikuchulia kutunza mazingira yanayozunguka maeneo ya mito mbalimbali inayoingia ziwani humo.

Hali jii imetokana na kuongezeka kwa shughuliza kibianadamu hussani za kiuchumi na kusababisha pia ziwa manyara kujaa udongo na matope pamoja uharibifu mkubwa wa mazingira.

Akiwasilisha mada kuhusu changamoto za uhifadhi katika hifadhi ya ziwa Manyara,Muikolojia katika hifadhi hiyo Bibi Christina Kiwanga amesema kukosana kwa utashi wa kisiasa ni changamoto kubwa katika kuliokoa ziwa hilo.

Bibi Kiwanga ametaja changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa mipango endelevu katika baadhi ya vijiji kuhusu umuhimu wa uhifadhi sanjari na elimu.

Muikolojia huyo amewambia wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha kwamba shughuli za Biandamu hususani za kilimo na za kiuchumi zimechangia kwa kiwango kikubwa hifadhi hiyo kuwa katika hatari ya kutoweka.

Naye Meneja Ujirani Mwema makao makuu ya Tanapa BWANA Ahmed Mbugi amesema umuhimu wa maeneo ya Mapito ya (SHOROBA) na mitawanyiko ya wanyama katika hifadhi amesema asilimia 80 ya Shooba zilizokuwepo miaka ya nyuma zimetoweka kabisa.

Amesisitiza kwamba ni lazima wananchi walinde uasilia wa mapito ya wanyama pori kutokana na umuhimu wa maeneo hayo Mbungi amefafanua kwamba awali kulikuwa na Maeneo ya SHOROBA yenye ukubwa wa ekari 40,000 katika hifadhi za Arusha Kilimanjaro,manyara lakii maeeo haya yamepungua.

Aidha amesisitiza kwamba wanasiasa wanachangia kuhujumu maeneo haya ya uhifadhi kutokana na kukosekana kwa kuchukuwa maamuzi mazito ya kuyalinda maeneo hayo kwa kuogopa wapiga kura hali inayoleta changamoto mbalimbali pindi wanapotoa taarifa za kulinda maeneo hayo.

Pia ameeleza kwamba asilimia 70 ya mapato yanayotokna na uhifadhi yanatumika katika usajidia utekelezaji w amiradi ya kijamii ikiwemo ya afya,elimu, maji, na miradi ya barabara.

Amesema migongano baina ya wanyamapori na binadamu inachangiwa na binadamu kuingilia maeneo ya mapito ya wanyamapori hivyo kuwakosesha njia za kupita hali inayoharibu mazingira.

Amesisitiza kwamba hatua hii inasababisha kuathiri shughuli za utalii ambapo idadi ya watalii hupungua sanjari na shughuli za uchumi kuathirika Mbali na hali hii katika kipindi cha mwaka 1957/63 na 1987/`988 uoto wa asilimia hususani misitu ulipungua kwa asilimia 13.5 wakati maeneo ya kilimo yaliongezeka kwa asilimia 10.9.

Aidha maeneo ya ushorobo yaliyotumika kwa shughuli za kilimo kati ya mwaka 1997/98 yaliongezeka kati ya asilimia 8.35 hadi 11.41 Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Lazaro Maasae yeye amesema kasi ya ziwa manyara kuendeleoa kujaa ugondo na matope ni ya kasi zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tanzania ni nchi ya ajabu kweli ivi hata hili la kutunza vilivyo vyetu wenyewe mpaka aje mtu mweupe?????Nani wa kulaumiwa ktk hili serikali au wasomi wataalamu wetu wa mazingira?Nina hakika tuna wataalum wengi tu wa mazingira wenye maelimu makubwa makubwa iweje washindwe kuishauri serikali cha kufanya juu ya hili na hata mengineyo kwa sehemu zingine????Mkapa juzi kasema sifa ya kumgundua mwenye elimu ni kwa kuona mambo mazuri ayafanyayo kwa jamii yake.Acheni kukaa mijini na kusubiri mwisho wa mwezi fanyeni kazi tembeeni muone watu wanavyoharibu vyanzo vya maji na mazingira kwa ukosefu wa elimu hili ni eneo lenu la kazi ikiwa pamoja na kuishauri serikali nini cha kufanya.

    ReplyDelete
  2. Msiwalaumu wasomi bure. Bila ushirikiano kati ya serikali, wasomi na wananchi wa kawaida hakuna kitakachofanyika. Serikali imeshikilia kila kitu. Msomi kazi yake ni kutoa mapendekezo. Je unafikiri hakuna mapendekezo yaliyotolewa serikali ikayapuuzia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...