Pichani ni   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mtunduru kata ya Isansa inajengwa kwa ajili ya kutunza mazingira na kuzuia upepo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi ambapo aliwaeleza kuwa CCM hii ni CCM inayofanya kazi na asiyeweza kufanya kazi na CCM hii awapishe,kwani wapo kwa ajili ya kutetea wakulima na wafanyakazi na si vinginevyo,aidha alisisitiza Vijana kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kwani ndio njia nzuri ya kuleta maendeleo na si kuamini kuwa Katiba mpya inaweza kubadilisha maisha yao.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dkt.Asharose Migiro akiwahutubia wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya.


 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Mbozi Ndugu Geofrey Zambi akihutubia wakazi wa Vwawa na kusema kuna matumizi mabaya ya pesa katika halmashauri za mkoa wa Mbeya na kusababisha kukwama kwa shughuli nyingi za maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...