Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa Tamasha la Krismas wametangaza kuwa tamasha hilo litafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu, pia litafanyika Mikoa ya Tanga na Arusha.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa baada ya kumalizika maonesho ya Dar es Salaam, Desemba 26 itakuwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Desemba 28 Uwanja wa Mkwakwani Tanga na siku inayofuata Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Alisema awali pia walipokea maombi kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wa Injili nchini wakiomba lifanyike katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na Mbeya, Mwanza, Shinyanga na Zanzibar.
“Kwa sasa tumepitisha mikoa hiyo minne, tunaomba wadau wetu watuunge mkono, tunaamini litakuwa tamasha la aina yake kutokana na aina ya wasanii tulio nao,” alisema Msama.
Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.
Kwa mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismas liwe bora zaidi kuliko la Pasaka kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania.
Alisema hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti kubwa iilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...