Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mmoja wa wanajumuiya ya Watanzania wanaoishi Mjini Seattle,Bibie Samia Mshangama mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Seattle kuanza ziara ya wiki moja ya Kiserikali Jimboni humo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Afisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani na Canada Mama Munaka Nje ya Uwanja wa ndege wa Seattle mara baada ya kuwasili.
Kushoto ya Balozi ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed, na kulia ni mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na wana jumuia ya Watanzani wanaoishi kwenye Mji huo Fatma Pazi na Samia Mshangama.
Mwanachama wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Seattle Ubwa Jaha akimfariji Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa uchovu wa safari wakati alipowasili Mjini Seattle kuanza ziara ya wiki moja.
Kulia ya Balozi ni Afisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Mama Munaka na kushoto yake ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Inter Connection cha clabu ya Rotary Mjini Seattle Bwana Charles Brennick akitoa ahadi Mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho ya kusaidia kompyuta kwa ajili ya Skuli za Zanzibar.
Kushoto ya Bwana Charles ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziar Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza mkutano wa dharura na wajumbe aliofuatana nao wa kupanga mikakati ya ziara yake ya wiki moja Mjini Seattle Nchini Marekani uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Marriot Mjini Seattle.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...