TAMASHA kubwa la filamu la kila mwaka la European Film Festival (EFF2013) lipo tayari kwa mwaka huu na litaanza rasmi tarehe 22 November 2013 kwa kuonyeshwa filamu mbalimbali katika vituo vilivyopangwa ambazo ni Alliance Francaise, Mlimani City Century Cinemax, Goethe-Institut na Nafasi ArtSpace filamu zitaonyeshwa kwa siku tatu tarehe 22, 23 na 24 November 2013.
Tamasha la hili limekusudia kuinua tasnia ya filamu ya Tanzania katika kujifunza utamaduni kutoka Ulaya katika njia ya filamu katika kuimalisha na kukuza utamaduni wan chi husika hivyo ni njia nzuri kwa watengeneza filamu wa Swahiliwood kushiriki katika kujifunza zaidi utengenezaji bora wa filamu.
Filamu nzuri na za kusismua kama vile Limbo, Kings, Tea or Electricity, The Great bear na nyinginezo zitaonyeshwa katika kujenga na kutoa nguvu sambamba na elimu burudani kutoka katika filamu husika, ni tamasha muhimu sana kushiriki kujionea tasnia kutoka Ulaya ilivyopiga hatua, KIINGILIO NI BURE


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...