CHUO kikuu cha usimamizi wa fedha IFM leo kimefanya mahafali yake ya 39 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Katika mahafali hayo ilishuhudiwa wanafunzi 3325 wakitunukiwa shahada, stashada na vyeti katika vitengo mbalimbali vivyotolewa katika chuo hicho.
Katika sherehe hizo mgeni rasmi Mheshimiwa Saada Mkuya alitoa zawadi mbalimbali huku Mhitimu Bilagi Paul Bilagi akiibuka kuwa mwanafunzi bora akiwa anasoma kozi ya masuala ya ukusanyaji kodi na kuzawadiwa shilling million moja(1,000,000) na mkuu wa chuo hicho.
Mwenyekiti wa mahafali hayo Profesa I.Jail amepongezwa na wazazi pamoja na wageni waliofika kiwanjan hapo kwa kuimarisha hali ya utulivu mpaka kufikia tamati ya mahafali hayo ya 39 mwaka huu.
Baadhi ya Wanafunzi wa IFM waliohitumu leo.
Meza Kuu.
Wahitimu.
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo hicho akipokea Cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafali hayo ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...