Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpa cheti
mwanafunzi Nuru Ally aliyefanya vizuri kuliko wanafunzi wote katika somo la
Development Studies katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kilichopo mjini
Morogoro. Mwanafunzi huyo pia alikabidhiwa zawadi ya Shilingi 50,000. Kushoto
ni Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma SUA, Profesa Peter Gillah.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahadhiri wa Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo
mbalimbali wanaotarajiwa kufanya mahafali yao kesho tarehe 29, Novemba 2013 katika
chuo hicho. Waziri Nchimbi alitoa vyeti
na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Kulia
ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Gerald Monela. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi
la Magereza (CGP) John Minja na Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Profesa Peter
Gillah
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wapili kushoto aliyevaa tai) wakiwa
katika picha ya pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja
na wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo mbalimbali wanaotarajiwa kufanya
mahafali yao kesho tarehe 29, Novemba 2013 katika chuo hicho. Waziri Nchimbi alitoa vyeti na zawadi kwa
wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...