Gari la kubeba Wagonjwa la Hospitali ya Manispaa ya Kinondoni likitafuta namna ya kupita kwenye Msongamano wa magari yaliyokuwa yamesimama nila mpangilio kwenye makutano ya barabara ya Shekilango, eneo la Sinza Afrikasana.
 hakuna gari inayoweza kusogea hata kwa hatua moja, maana magari yamesimama bila hata mpangilio.
 wengine ndio wanazidi kutania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Dar Es Salaam kuna ongezeko la magari ambayo ni tatizo moja wapo linalosababisha foleni. Lakini kwa upande mwingine foleni inasababishwa na uzembe wa madereva hasa daladala ambao wengi wao wana elimu ndogo. Lakini ni vema kuendekeza uzembe huu? Ki-msingi madereva wako juu ya sheria kwani wanaendesha magari wanavyotaka na wakati mwingine askari usalama huwa wanakaa pembeni wanaangalia tu. Serikali haina budi kuweka sheria kali katika hili. Magari yameongezeka, hali kadhalika pato la serikali kwa tozo mbali mbali za kodi inayotokana na magari; hivyo basi nguvu kazi ya usalama barabarani nayo iongezwe. Kama kikosi cha usalama barabarani kimelemewa, FFU isaidie. Pili adhabu mbadala itafutwe kwa ajili ya madereva wakorofi. Napendekeza kikosi cha JKT kihusishwe hasa hawa new recruits. Madereva wanaotanuwa, wasimamishwe kwa masaa matatu na sio chini ya hapo. Utafutwe uwanja wa wazi, au kama service road waliotanuliwa haipo busy, wawekwe hapo kwa masaa matatu. Kwa upande wa JKT wao watakuwa wanatekeleza zoezi la gadi. Baada ya hapo madereva wapigwe faini. Asilimia fulani iende JKT. Aidha jopo la wanasheria na askari usalama waketi pamoja watafute adhabu nyingine mbadala. Penye nia pana njia. Naomba sana Kaka Michuzi upeleke maoni haya kwa wahusika

    ReplyDelete
  2. Naomba Kaka Michuzi uwasilishe ombi letu watumiaji wa barabara ya Sam Nujoma nyakati za jioni. Tunaomba huduma ya askari wa barabarani pale kwenye njia panda ya kwenda chuo kikuu na Sam Nujoma road, karibu na daraja la ubungo. Ni kero usisikie. Kuna wale wanotanua kwenye service road za pande zote mbili, foleni, vurugu. Matokeo yake watu wanasema trafiki ubungo anapendelea upande mmoja, kumbe wala sivyo, ni ile vurugu pale ndio inasababisha msururu mrefu. Aidha tunaomba blocks kubwa za concrete ziwekwe katika zile service roads kwani, service roads hizo hazitumiki sana na hizo blocks au vizuizi havitazuia shughuli zozote za kimaendeleo. Sehemu ile imekuwa kama jinamizi. Ukifika pale, kwa sisi Wana Mama lazima tusali kwanza. Naomba uwasilishe maoni haya kwa wahusika. Nakufagilia sana kwa kazi nzuri ya kuwakilisha maoni ya jamii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...