Sehemu ya viti vilivyong'olewa katika  stendi inayokaliwa na mashabiki wa Simba uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya mchezo wao na Kagera Sugar Wekundu wa Msimbazi walipotoka sare ya 1-1 na kutokea vurugu kubwa. Je, huu ni uungwana???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hapo tatizo lipo kwenye serikali yetu isiokua na maamuzi magumu ndio maana mijitu mijinga inafanya itakavyo,,kama mm ningekua kiongozi wa wizara inayohusiana na hiyo michezo hakiyamungu hao woote waliohusika NINGEWAFUNGA MAISHA GEREZANI,,nahuko Gerezani kazi yao ingekua ya kufatua matofari ya kujengea shule za vidudu ili watt wetu waelimike zaidi,,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UINGEREZA,,maana ukisikia ushetani ndio huo,,nawapendeni woote huko nyumbani kasoro hao MASHETANI wasio na woga wala haya,

    ReplyDelete
  2. Huu ni ushabiki wa kishamba sana...watu walioenda shule hawawezi kufanyi vitu kama hivyo....unajiuliza ni kwa vipi kuvunja viti kunaweza kubadilisha matokeo ya mchezo....kama timu yako imeshindwa kufanya vizuri kama ulivyotarajia huo siyo mwisho wa maisha mpira utaendelea kudunda shida iko wapi mpaka mnatuharibia miundombinu ya uwanja wa gharama kama huu?

    ReplyDelete
  3. Mnyama mnyama tu kashazoa pori na vichaka ukimleta mjni anaparamia kila sehemu. Serikali imejenga uwanja Watz waangalie soka kwa starehe alaf watu wanafanya MAKOROKOCHO LAZIMA WATAKUWA WANYAMA HAO.
    Wasimizi wa uwanja na shauri kuboresha security ili WANYAMA kama hao wanalipa fidia hapo hapo. Tickets ziongezewe precaution note ya kumuwajibisha mtu atakae atakae haribu vifaa vya uwanjani

    ReplyDelete
  4. Klabu ya Simba ilipe garama za Kukarabati hivyo viti!

    ReplyDelete
  5. Samahani waungwana, lakini haya nilishayasema toka zamani kuwa, sielewi ni vipi watu na akili zao wanatoka kwao kuja kuvunja vyoo vya uwanja wa Taifa?!, uwezi kabisa kuingia vyoo vya pale Taifa. Haya sasa ona jamaa wanavunja viti. Narudia tena, sio viongozi na wala sio marefaa, bali siye watu inabidi tubadilike. Tukibadilika na viongozi watafuata, kwani viongozi ni watu kama sisi. Viongozi wenye hekima wanawafundisha wachezaji wao na mashabiki wao kuwa na hekima. Ndugu zangu Watanzania wakati ndio huu naomba tubadilike kwa kuwa na mwenendo mzuri. Uwanja wa taifa uwezi ukaenda na mke wako au mtoto kuangalia mpira kama tunavyofanya mataifa yaliyoendelea, hii ni aibu.

    ReplyDelete
  6. tushirikishe ubongo tunapofanya maamuzi... Uungwana ni vitendo

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. Hatujafika mahala pakuwekewa viti. Tunahitaji mabenchi ya zege!!

    ReplyDelete
  9. Dcnyarugusu sio Asira ni Hasira . Pia Asara ni hasara.

    ReplyDelete
  10. Msimbazi mambo hayo ya uharibifu wa mali mngefanyia Klabuni kwenu!

    Hizi ndio Bange za Mtaa wa Msimbazi?

    Oysterbay Ukumbi wa Polisi mlimaliza kikao kwa amani na mkaondoka mikono nyuma kimyaaaa!

    Mbona Mkutano wenu mlipo ufanyia Ukumbi wa Polisi Officers Mess Oysterbay hata sigara sio kuvuta ile tu kuwasha mliogopa?

    ReplyDelete
  11. Sababu ni kukosekana kwa adhabu kali kwa mashabiki na club yao lakini pia kukosekana kwa kamera za usalama maana ilitakiwa hao wahusika wote watambuliwe na kukamatwa na kupewa adhabu stahiki.

    ReplyDelete
  12. Hivyo viti, vilipwe na club ya Simba iliwaelewe kukemea mashabiki wao. Nilikuwa mpenzi wa saimba, sitaki tena mpumbavu huo, timu inawashaki wajinga hivyo. Ulinzi uimarishwe hapo taifa ikiwa ni pamoja nakuchukua hatua kwa wapumbavu hao. Aidha, kiingilio kiwe kuanzia elfu hamsini ili wanaoenda huko wawe ni wale wastarabu. Uwanja wa Taifa pia utumike kwenye michezo maalum tu na siyo hiyo ya kipuuzi. Ili hao wapuuzi wakatazamie huko mchangani maana hawastahili hapo. Suala hili lijadiliwe kwa kiina kitaifa na litungiwe sheria maalumu kwa ajili ya udhibiti, Wizara ya michezo mpo na mnaona haya wala msichukue hatua kweli????

    ReplyDelete
  13. aidha Simba Sc ilipe harama, au wafungie washabiki wa Simba au wawatowe wale ambao walihusika na unyama huu ili sheria ifate mkondo wake. Simba kama club inawajibika kwa vitendo vya washabiki wao. Mnyama ni Mnyama tu huenda wakibadili jina watabadilika, labda sasa waitwe mbuzi jike

    ReplyDelete
  14. Huuni ujinga, ambao mtu unabaki speechless, yaani mtu na akili zako kabisa,unafanya vitendo vya kijinga kama hvi, sasa siku nyingine mpira au timu yenu ikicheza utakaa wapi? atujielewi sisiwafrica kila siku ni hovyo hovyo, hatujui hata vitu vizuri wala vibaya, sasa waweza kukuta kundi hilo ni la lile wasioenda hata shule, zaidi wao wanachojua ni simba na yanga tu, na vurugu basi, hata majumbani mwao wanakotoka wametopea Kwa umasikini, na wengi wetu humo majumbani hata vitanda hawana, wala hawajielewi, ndio maana, hawajui kizuri wala kibaya, kwao sawa tu. mradi sifa kwao, kwamba wamechukia wameharibu Kwa kuwa vichwani mwao umejaa ujinga mtupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...