Mfungaji wa mabao mawili ya timu ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Mrisho Ngasa akishangilia bao lake la kwanza katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanjawa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeshinda mabao 4-0, mabao mawili yakifungwa na Mrisho Ngasa, katika dakika za 4 na 23 kipindi cha kwanza, bao la tatu limefungwa na Oscra Joshuo, katika dakika ya 50 na bao la nne limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 86. Picha na Francis Dande
 Mshambulijia wa Yanga, Hamis Kiiza akiwa katika harakati za kufunga.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia.
Beki wa JKT Ruvu akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Kiungo wa JKT Ruvu, Nashon Naftal akimtoka Mrisho Ngasa.
Simon Msuva akichuana na Kessy Mapande wa JKT Ruvu.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la tatu lililofungwa na Oscar Joshua.

 Mshambuliaji wa Yanga, aliyeingia kuchukua nafasi ya Didier Kavumbagu, Jerry Tegete, akimtoka beki wa Ruvu JKT , Nashon Naftal, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni hii. 
 Jerry Tegete (kushoto) akishangilia bao lake kwa staili ya kunong'oneza, huku akipongezwa na Simon Msuva (kulia) na Mrisho Ngasa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera yanga,hongera mashabiki wa yanga kwa kushangiria kwa utulivu bila ya kuacha athari uwanjani.

    ReplyDelete
  2. Ohoo mbona Mabao mengi namna hiyo?

    Kama mpo kwenye Basketball au Netball vile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...