Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Prof. Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO).

Rais pia amemteua Bwana Freddy Safiel Manongi kuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ambaye hivi sasa ni kaimu Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori cha Mweka na pia amemteua Prof. Audax Zephania Philip Mabula kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.

Uteuzi huu umeanza rasmi mwishoni mwa Mwezi Oktoba mwaka huu.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana prof kwa uteuzi huo, lakini una kibarua kizito cha kufanya mageuzi makubwa ya kiutendaji na kimfumo.

    ReplyDelete
  2. Prof Madundo si DVC pale Nelson Mandela Institute of Technology??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...